Burudan Mwanzo - Mwisho

Monday, February 25, 2013

MAPACHA WATATU KUTOA ALBAM YAO MPYA MARCH 2


Na Super D

BENDI ya Mapacha watatu ipo mbioni kuzindua albam yake ya pili itakayokwenda kwa jina la yarabi nafsi baada ya ile ya kwanza iliyokwenda kwa jina la jasho la mtu

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi huo meneja wa bendi hiyo Hamis Dacota amesema kuwa uzinduzi uhuo utafanyika katika ukumbi wa Businness Park Victoria March 2 na kusindikizwa na wasanii Linah Sanga, Khadija Kopa na bendi ya Mashujaa

Albam hiyo itakayokuwa na nyimbo nane kama Yarabi Nafsi, Usia wa babu, chanzo wanaume, naonewa, wajasilia mali, wivu na Sumu ya Mapenzi rimix

aliongeza kwa kusema kuwa wamechukua vipaji vipya vya muziki ambao wataonekana kwa mara ya kwanza katika albam hiyo aliwataja wasanii waliowaongeza kuwa ni Catherine Fidelic ' Cindy' John Cene na Twaha Makopa ambao wamewapika na kuiva kwa kutoa burudani

Mbali na kuzindua albam hiyo watatoa CD moja ya bule mlangoni kwa kili mshabiki atakae kata tiketi kwa siku hiyo ya uzinduzi alisema Dacota
Super D (Mnyamwezi) at 11:46 PM

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version
Powered by Blogger.