Mwenyekiti wa CCM Rais Janakaya Kikwete akiongoza matembezi ya
maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, leo asubuhi kutoka eneo la Mnarani hadi
ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma leo. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Philip Mangula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani
Kaborou, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
(kulia)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza
matembezi ya mshikamano ya Miaka 36 ya CCM, mjini Kigoma leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya Mshikamano ya Maadhimisho
ya Miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo
Matembezi hayo yakipita eneo la Burega, Barabara ya Kigoma-Ujiji
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa na Mwenyekiti wa
Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Kigoma
Jumanne Maneo
Wananchi wakishangilia wakati matembezi yakipita barabara ya Ujiji Kigoma kwenda Ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili eneo la Mnarani mjini Kigoma tayari
kwa matembezi hayo. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara),
Philip Mangula na wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu
Nchemba na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose
Migiro
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi
msafara wa matembezi hayo ulipokaribika kufika Ofisi ya CCM mkoa wa
Kigoma
Rais Kikwete akiwa na Nape na Kinana baada ya msafara wa matembezi hayo kuwasili
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikweye akiwa na muaasisi mmoja wa CCM ( ambaye
jina lake halikuweza kupatikana mara moja) baada ya matembezi kufika
Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
Mama Salma Kikwete akisalimia baada ya msafara wamatembezi hayo kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na msafara wake wakiwa wameketi meza kuu Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma baada ya matembezi hayo.
"NDUGU WANANCHI, NAWAPONGEZA KWA KUSHIRIKI KWA WINGI KWENYE MATEMBEZI
HAYA. HAPA SISEMI MENGI TUKUTANE MCHANA PALE UWANJA WA LAKE TANGANYIKA"
Akasema Rais Kikwete wakati akizungumza na wananchi baada ya matembezi
hayo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO@Daily Nkoromo Blog)
No comments:
Post a Comment