Monday, March 11, 2013

Benki ya Exim yafungua tawi jipya mjini Shinyanga



Mkuu wa Mkoa Shinyanga Ali  Lufunga (wakwanza mbele) akikata utepe kuzindua tawi jipya la Benki ya Exim ya Tanzania mjini Shinyanga mwishoni mwa wiki. Nyuma yake kushoto ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo Anita Goshashy. (Na Mpiga Picha Wetu)

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga

BENKI ya Exim Tanzania imepiga hatua nyingine kwa kufungua tawi jipya mjini Shinyanga ikiwa ni kutekeleza mpango wa benki hiyo wakufikisa huduma za kibenki katika maenoe mbali mbali nchi.
Benki hiyo kwa sasa imefikisha idadi ya matawi 25 nchi nzima huku ikitarajia kufungua mwtawi mengine kwenye mikoa ya Tabora, Arusha and Dar es Salaam kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo jipya mjini Shinyanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Tanzania, Bw. Anthony Grant alisema kuwa ufunguzi wa tawi hilo jipya unaonyesha dhahiri jitihada za benki hiyo kufikisha huduma zakibenki kwa wananchi waliopo pembezoni mwa nchi.

Grant alisema kuwa benki yake kwa sasa imejikita katika mpango wa kutanua huduma zake wenye lengo la kuhakikisha kuwa benki inafungua matawi mapya katika maeneo yasiyoweza fikiwa na benki nyingine kabla ya mwisho mwa mwaka huu.

“Dhamira ya Benki ya Exim ya kuongeza mtandao wa matawi yake unaonyesha jitihada ya benki yetu kufikia wananchi wengi nchi nzima. Tunafuraha sana kufungua tawi hili mjini Shinyanga kwa kuwa linazidi kuimarisha huduma zetu nchini. Tawi la Shinyanga ni uthibitisho wa jitihada zetu za kufikisha huduma za kibenki karibu na watu.
“Mkoa wa Shinyanga una vivutio vingi vya kibiashara na unahitaji huduma za kibenki zilizobora; na kwa sababu hizo benki ya Exim itaendelea kuwekeza kwenye tafiti mbalimbali ilikutoa huduma za kipekee zinazolenga makundi mbali mbali hapa nchini,” alisema. 

Grant alisema benki yake imejikita katika kusaidia kukuza wafanyabiashara wadogo na wakati (SMEs) nchini Tanzania kwa kuelewa kuwa biashara ndogo ndogo na za kati ndiyo chachu ya kukuza uchumi endelevu.

“Biashara ndogo ndogo za kati bado ni nguzo kuu ya uchumi wa nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Benki ya Exim itaendelea kusaidia wafanyabiashara wadogo na wakati nchini kupitia bidhaa/huduma maalum zinazokidhi mahitaji yao,” aliongeza Grant.

Naye Mkuu wa Mkoa Shinyanga Ali  Lufunga wakati wa hafla hiyo aliwaasi wananchi wa  mkoa huo kuchangamkia fursa mbali mbali zitakazopatikana na ufunguzi wa Tawi la Benki ya Exim mjini Shinyanga.
“Uamuzi wa benki ya Exim kufungua tawi jipya mjini hapa ni ishara tosha kuwa benki hii ina imani na mkoa wetu.

“Wananchi, tuache mambo ya kizamani ya kutumia vibubu na tuanze utamaduni wa kuweka fedha zetu benki,” alisema Lufunga.

No comments:

Post a Comment