NA BASHIR NKOROMO
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana anaondoka nchini leo Machi 10, 2013, kwenda Jamhuri wa Watu wa China kwa ziara ya kikazi ya siku kumi, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) cha nchi hiyo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk.
Asha-Rose Migiro amesema leo kwamba katika ziara hiyo Kinana atakuwa
na msafara wa watu 14, ambao baadhi yao ni Wajumbe wa Kamati kuu ya
CCM, Makatibu wakuu wa Jumuia za Chama na Wenyeviti wa Chama wa mikoa.
Akizungumza
leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam, Dk.
Asha-Rose alisema, Kinana na msafara wake wanatarajiwa kufika Guangzhou
China keshokutwa, Machi 12, 2012.
Alisema,
ziara hiyo ambayo ni ya kwanza nje ya nchi kwa Kinana tangu kuteuliwa
kwake kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Oktoba, mwaka jana,
imeandaliwa
na Chama Cha Kimomunisti cha China kwa lengo la kupata fursa ya
viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo kubadilishana uzoefu katika
nyanja mbalimbali za kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya vyama na
wananchi wa nchi Dk. Asha-Rose alisema baada ya kuwasili Guangzhou,
kinana na ujumbe wake wakiwa na wenyeji wao wa Chama Cha Kikomunisti cha
China watatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo jiji la Dong-guan,
Shenchen, Chengdu, Machi 13-14, 2013, msafara utakwenda jiji la Chengdu,
Sichuan, Nanchong na kumalizia ziara hiyo katika jiji la Beijing ambako
atawasili Machi 18, 2013.
Tanzania
na China zimekuwa na uhusiano wa siku nyingi katika maeneo mbalimbali
yakiwemo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni na pia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Kimkomunisti cha China (PCP) ambavyo ni
vikongwe vimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia kwa miama mingi na
uhusiani huo uanelezwa kuendelea kukua na kuimarika siku hadi
siku.Ushirikiano unaoonekana kuwa wa kindugu wa nchi hizo za Tanzania na
China uliasisiwa tangu enzi za waliokuwa viongozi wa nchi hizo,
Hayati
Baba wa Taifa Julius Nyerere na Mao Tse Tung.Moja ya miradi
inayotghibitisha uhusiano na urafiki wa kindugu baina ya China ya
Tanzania, ni mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya TAZARA na maradi wa
TAZAMA, Mradi wa zana za Kilimo Ubungo, mradi wa kiwanda cha Mang'ula
na wa kiwanda cha nguo cha urafiki.
No comments:
Post a Comment