Washiriki wa shindano la Miss Utalii Tanzania Fainali za Taifa 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Ukumbi wa Dar Live.
Washiriki
wa Miss Utalii Tanzania Fainali za Taifa 2012/13 wakiwa katika mazoezi
ya nguvu ya kujiandaa na Shindano lao la Vipaji ndani ya Ukumbi wa Dar
Live.

***************************
Shindano
la Taifa la Miss Utalii Vipaji 2012/13 linafanyika kesho katika ukumbi
wa Dar Live Mbagala, ambapo Warembo 40 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar
na Kanda Maalum vyuo Vikuu Tanzania , watapanda stejini kushindana
kucheza Ngoma za asili kutoka Mikoa ambayo wanawakirisha,watapita na
mavazi mbalimbali.
Katika
shindano hilo mbali na Burudani kutoka kwa Warembo wa Miss Utalii
Tanzania 2012/13 kutakuwa na Burudani zaidi za Ngoma za Asili, Muziki
wa kizazi Kipya pamoja na Burudani kutoka kwa Mwanamuziki wa Kimataifa
Che Mundugwao, Atakuwepo pia mwanamuziki chipukizi wa Bongo Flava Dogo
Genius ambeye ametokea kuwa mpinzani mkubwa wa Dogo Janja na Asley.
Shindano
hili ni la awali ambalo litapata Mshindi wa Vipaji kabla ya kufanyika
fainali kuu ambalo litampata Miss Utalii Tanzania litakalo Fanyika
Tarehe 17.03.2013 katika ukumbi wa Dar Live. Mshindi wa Tuzo hilo la
Vipaji atajipatia zawadi ya Kusomeshwa Bure katika ngazi ya Cheti au
Diploma kulingana na Sifa zake. Mshindi wa Mwaka jana na ambaye
anashikiria taji Hilo kwa sasa ni Daisy Msumbusi Miss Utalii Kutoka Mkoa
wa Kagera.
Katika
Shindano hilo , ulinzi utakuwa umeimarishwa ambapo kutakuwa na Polisi
na Ninja, usalama wa Magari pamoja na vitu vyote utakuwa ni wakutosha,
kutakuwa na eneo la kutosha la kuegesha Magari na walinzi muda wote
watakuwepo katika eneo hilo.
Viingilio katika Shindano hilo itakuwa kama ifuatavyo, Viti vya kawaida Tsh 5,000 na Viti Maalum 10,000
Fainali
za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana
Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza,
VAM General Suppries Limited,Michuzi Media Group,Global Publishers,
TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv,
Vailey Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la
sanaa la Taifa (BASATA)
No comments:
Post a Comment