Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 7, 2013

MKURUGENZI MKAZI WA SHIRIKA LA KIJERUMANI LA FRIEDRICH EBERT STIFTUNG LINALOJIHUSISHA KATIKA KUJENGA DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA AMTEMBELEA WAZIRI NCHIMBI OFISINI KWAKE.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza jambo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkazi mpya wa Shirika la Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung linalojihusisha katika kujenga Demokrasia na Utawala Bora, Rolf Paasch (kulia). Katikati ni Mkurugenzi Mkazi ambaye amemaliza muda wake kulitumikia shirika hilo nchini, Dk. Stefan Chrobot. Mkurugenzi Mkazi huyo mpya na aliyemaliza muda wake wamemtembelea Waziri Nchimbi kwa lengo la kujitambulisha na kumsalimia.
Mkurugenzi Mkazi aliyemaliza muda wake kulitumikia Shirika la Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung nchini linalojihusisha katika kujenga Demokrasia na Utawala Bora, Dk. Stefan Chrobot akimfafanulia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) masuala mbalimbali kuhusiana na shirika lake. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi mpya wa shirika hilo, Rolf Paasch.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung linalojihusisha katika kujenga Demokrasia na Utawala Bora. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi ambaye amemaliza muda wake kulitumikia shirika hilo nchini, Dk. Stefan Chrobot. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi mpya wa shirika hilo, Rolf Paasch.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...