FOR IMMEDIATE RELEASE – Friday, March 8th, 2013-Dar-Es-Salaam, TANZANIA- Richard
Commey amedhihirisha uwezo wake wa upigana ngumi wakati alipomtoa kwa
TKO bondia Bilal Mohammed na kutangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi
katika bara la Afrika. Mpambano huo ulifanyika katika ukumbi wa Wills
Gym City Engineers katika viunga vya Jamestwon, jijini Accra, Ghana na
kuhudhuriwa na wapenzi wengi wa ngumi wakiongozwa na viongozi waandamizi
wa Chama cha Ngumi cha Ghana (GBA), viongozi wa Kamati ya Olympic ya
Ghana, Meya wa jiji la Accra, pamoja na wWaziri wa Michezo wa Ghana.
Mpambano
huo ulianza kwa mbwebwe za aina yake baada ya mabondia wote kuwasili
kwenye ulingo wakisindikizwa na mashabiki wao waliokuwa wanacheza ngoma
mbalimbali za makabila ya Ghana.
Bilal
alianza mpambano katika raundi ya kwanza akikurupuka kutoka kwenye kona
yake kama faru na kumfuata Richard kwa nia ya kumsimamisha katika
raundi ya kwanza lakini Richard aliweza kuhimili shambulio hilo na
kuanza kutoa dozi kwa Bilal.
Katika
raundi ya 4 Richard alimpeleka Bilal kwenye sakafu ya ulingo mara mbili
kwa ngumi zilizokuwa nzito. Bilal aliweza kuendelea na pambano baada ya
kuhesabiwa mara 8! Mashabiki wengi aliuzingira ulingo wakati wote wa
mpambano huku wakipiga makalele na ngoma zilizoashia kuwa wawili hao
kweli wametawala nyoyo za mashabiki wengi wa ngumi katika nchi ya Ghana.
Mambo
yalifikia tamati katika raundi ya saba wakati Richard aliporusha ngumi
tatu mfululizo za mchanganyiko na kumpeleka Bilal chini kwa mara ya
tatu. Bilal aliamka kwa shida wakati mahesabu ya refarii yalipokuwa
yanafikia mwisho na alianza kupepesuka huku refarii akimdaka ili
asianguke tena na kuashiria mwisho wa mpambano huo.
Huu
ni wakati ambapo Richard Commey alipotangazwa kuwa Mfalme wa uzito
mwepesi katika bara la Afrika na ukumbi mzima kuzizima kwa nderemo na
shangwe. Kwa ushindi huo, IBF imempatia Richhard Commey nafasi ya
kuwania ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito mwepesi mpambano ambao
utafanyika tarehe 28 mwezi wa Aprili mwaka huu.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment