Saturday, March 9, 2013
TANZANIA YANG’ARA NA VIVUTIO VYAKE VITATU MAONYESHO YA (ITB) BERLIN UJERUMANI
Wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakigonganisha glasi za mvinyo wa matunda ya Mananasi uliotengenezwa nchini Burundi wakati wa hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)kwenye maonyesho ya utalii ya (ITB) yanayofanyika kwenye jengo la Mense Berlin jijini Berlin Ujerumani, Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na mkakati wa Kutangaza utalii wa Afrika Mashariki na mwaka huu ilikuwa na kazi moja ya kunadi maajabu manne ya Afrika yaliyopatikana katika ukanda huu wa nchi za Afrika Mashariki ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mto Nile, Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro Crater huku Tanzania ikiwa kinara kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa maajabu yake matatu ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Serengeti na Ngorongoro Crater jambo lililofanya itamkwe mara nyingi miongoni mwa viongozi waliopata nafasi kuzungumzia utalii wa Afrika Mashariki PICHA NA FULLSHANGWEBLOG
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akipokea tuzo maalum iliyotolewa na iliyotolewa kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Bi Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda katika hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye maonyesho ya (ITB) Berlin jana, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa (EAC) Jesica Eriyo
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Meena kulia akiwa na Adolf Mchemwa Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania Ujerumani wakiwa katika hafla hiyo
Bi. Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hotuba yake na kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu utalii wa nchi za Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment
‹
›
Home
View web version
No comments:
Post a Comment