Monday, April 1, 2013

TIMU NNE ZITAINGIA KATIKA KIPINDI CHA TATU KUCHUANA VIKALI WIKI HII, NI KATIKA SHINDANO LA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ MSIMU WA TATU (3)


Episode 3 team- bloggersTimu nne zitakazochuana katika kipindi cha tatu cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kuanzia kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania –bluu, Uganda- kijani na nyeusi ni timu kutoka Kenya. TamashaMeneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi(kulia) na mtangazaji wa kipindi cha Tamasha la michezo Amry Masare wakijadili na kufanya uchambuzi wa kipindi cha kwanza na pili cha Guinness Football Challenge jana katika kipindi cha Tamasha la michezo kinachorushwa na televisheni ya ITV.
………………………………………………………………
Jumatano iliyopita  kupitia televisheni  za ITV na Clouds TV mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalituonesha ni kwanini ushirikiano ni muhimu kwa  washiriki kuonyesha ujuzi wao. Francis Ngigi and Kepha Kimani kutoka Kenya walifanikiwa kuingia hatua ya mwisho  na kujipatia fedha za kimarekani  dola 3,000 shukrani kwa vipaji vyao na ushirikiano mzuri.
 Francis na Kepha wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.
 GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .
 Katika Episodi ya tatu ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana siku ya Jumatano.
 Hizi ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha pili wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.
Timu ya bluu-Tanzania:
  • Mohamed Kobembe na Gullam Sosha wenye umri  wa miaka 23 kutoka Dar es Salaam watashirikiana kuona kama wataweza kushinda katika kipindi cha tatu cha GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.Mohamed ndiye kichwa cha timu ni mwanafunzi  wa  shahada ya kwanza ya maswala ya kodi na Gullam ambaye ni mchezaji wa Ndanda FC, wana matarajio ya kufanya vizuri katika mashindano hayo. 
 Timu nyekundu-Kenya:
  • Kenneth Kamau mwalimu wa timu ya vijana(23) na Willis Ogutu(miaka 30) wote kutoka Nairobi watachezea Kenya.Keneth ataonesha maarifa yake ya soka  wakati Willis ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira.
 Timu ya kijani-Uganda:
  • Kennedy Mwota(22) kutoka Naijanakumbi na Steven Nsubuga(25) kutoka Kampala.Kennedy ni mwanafunzi na Steven ni muhasibu.Kennedy ataonesha ujuzi wa soka  na steven kipaji chake cha kusakata kabumbu.
 Timu nyeusi-Kenya:
  • Wafanya biashara wa Nakuru,Stephen Kaguda,35 na Gideon Onyango,34, watavaa jezi meusi. Stephen ambaye ni mshabiki wa Barcelona FC atakuwa akijibu maswali wakati Gideon ambaye ni mshabiki wa Man Utd atachezea mpira.
 Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu.   Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.  
 Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya, Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufatilia  ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.
 GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.
 Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya  Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 
 *Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.  Tafadhali Kunywa kistarabu.

No comments:

Post a Comment