Tuesday, May 7, 2013

Taswa FC, Taswa Queens kuumana na Bongo Movie Jumamosi



Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na timu ya netiboli, Taswa Queens Jumamosi zitacheza na timu ya wacheza filamu, Bongo Movie FC na Bongo Movie Queens katika mchezo maalum wa kirafiki.
Mechi hizo zimepangwa kufanyika kwenye uwanja wa TCC, Chang’ombe kuanzia saa 10.00 jioni kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa mchezo wa kwanza ambao utahusisha timu za netiboli umepangwa kuanza saa 10.00 jioni ambapo  siku hiyo Taswa Queens itakuwa ikicheza mechi yake ya tatu tokea kuanzishwa kwake siku ya sikukuu ya Pasaka mwaka huu.
Mechi ya kwanza ya Taswa Queens ilikuwa dhidi ya Kiliflora Queens na kushinda kwa mabao 28-8 na mechi ya pili ilikuwa dhidi ya Kombaini ya walimu wa wilaya ya Kibiti na kushinda kwa 36-2.
Majuto alisema kuwa wachezaji wa Taswa Queens chini ya wachezaji wake, Imani Makongoro na Oliver Albert,  kutoka Mwananchi Communications Limited aliyechezea nafasi ya GA, Clezencia Tryphone (Tanzania Daima), Elizabeth Mbassa, Sharifa Mustapha na Johari William wote wa  Business Times Limited (BTL). Makocha wao ni Amina Mussa  kutoka BTL na Zainabu Mussa.
Kwa upande wa Taswa FC, mechi hiyo ni muhimu sana kwao kutokana na matokeo mabaya ya mechi ya mwisho ya kufungwa mabao 2-0 wilayani Kibiti.
Majuto alisema kuwa wamejiandaa vizuri ili kutoa kipigo kwa Bongo Movie katika siku hiyo ambapo bendi ya Msondo  itatumbuiza baada ya mchezo huo ulioandaliwa na Dar Bonanza.
“Mechi zote mbili ni sehemu ya maandalizi yetu ya safari ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga, hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kushinda, makocha wangu, Ali Mkongwe na Ibrahim “Maestro” Masoud wameandaa programu nzuri na bila shaka itatoa matunda mazuri,” alisema Majuto.

No comments:

Post a Comment