Saturday, June 22, 2013

KAULI YA PINDA; ASIYETII PIGA TUMECHOSHWA ITAMLIZA TENA?



‘Ngariba ukimpa mtoto atamfanya vyoyote atakavyo’

Na Bryceson Mathias

KUTOKANA na watanzania nchini kupoteza Imani na Jeshi la Polisi kila Kona ya nchi, kuwa linakisaidia Chama Tawala (CCM), huenda Kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kulipa Jeuri Jeshi hilo kuwa, liwapige tu wasiotii amri waumechoshwa; litamsababishia kulia Tena!.

Kauli ya Pinda imesemewa mahali palepale aliposemea awali kuhusu wanaoua walemavu wa Ngozi (Albino) kuwa nao wauawe, na alipogeuziwa kibao na watoa hoja wa eneo hilo hilo aliloko, alilia kwa uchungu na kujutia Kauli ya Ulimi wake, jambo linaloonesha litamrejea!

Kwa kuwa Pinda ni Msimamizi Mkuu wa Shughuli za Serikali bungeni, wananchi hawaoni kama Pinda kasema, ila wanatafsiri kwamba hiyo ndiyo Kauli ya Serikali ya sasa na Muundo wake (Mfumo), na kuwa sasa itakuwa mtu asipotii Sheria bila Shuruti ni kupiga tu! Tumechoka!.

Lakini kibaya kinachojitokeza, Pinda katamko kauli hiyo nzito kwenye chombo kikuu cha kutunga sheria kati ya Mihimili mitatu (Utawala, Mahakama na Bunge), hivyo watu wanahisi Taswira hii; ‘Kama anaweza kutoa Kauli hiyo nzito hadharani, akiwa kwenye vikao vya siri Je!

Wadau wengi wanapohojiwa Sirini ni wapi wanadai, Kwenye Vikao vya Mikakati ya Uongozi ndani ya Itikadi yake, Halmashauri Kuu, Kamati Kuu, huku wengine wakisema, Pinda hajui Ugeugeu wa Polisi, linaweza kuanza utekelezaji kwa nguvu wakisingizia kasema Waziri Mkuu.

Jambo kubwa linalowauma watanzania wengi waliosikia Kauli ya Pinda na Michanngo mbalimbali, hasa baadhi ya Wasomi na Watalaam wa Uchumi wanasema,”Pinda katoa Kauli hiyo wazi mno, na kwamba, Vyombo vya Habari na vya Haki vya Kimetaifa vimemsikia.

“Awali Waziri, Bernard Membe, alilalai ati kuna watu wanadiriki kushawishi Wawekezaji Nje, ili inyimwe misaada kwa kukosa uzalendo na nchi yao”. Wanahoji, kwa tamko la Pinda, Wawekezaji wakisitisha Misaada Tanzania, Mchawi ni Nani?
Pia ni hofu ya watanzania kwamba, Kama mtu ukimkabidhi Ngariba mtoto; humfanya anavyotaka, hata mtoto akilalamika kufanyiwa sivyo ndivyo, huambiwa hatii sheria za Jandoni!

Upo uwezekano mkubwa na hata Polisi huenda wakaitumia vibaya amri ya Pinda wakidai, wao ni ndio Afande hakuna kuuliza, na kwa hiyo watawapiga wananchi ovyo, kwa madai wanatekeleza maagizo, mtu asipotii sheria pasi shuruti, Pinda aliagiza Piga tumechoshwa!

Utekelezaji mbaya wa kauli hiyo, itafika mahali utaleta madhara, kwa sababu wananchi watapigwa na baadaye nao watachoshwa na vipigo vya Polisi, na kusema inatosha, tumepigwa kiasi cha kutosha, tumeonewa kiasi cha kutosha, na unyonge wetu ndio uliotufikisha hapo, basi! Enough is enough.

Baaadhi ya wasomi wa Uchumi Mzumbe Morogoro walisema, Awali walizoea kusikia Ugonjwa wa Upofu wa Macho upo Mikoa miwili nchini! Lakini wanadai, sasa nchi nzima watu watakuwa vipofu, wenye miwani.

Wanadai sababu kubwa macho ya watoto Shule yataharibiwa kwa mabomu ya machozi, Maji ya kuwasha na Moshi, kutumika na kuhatarisha afya zao bila sababu za msingi, ambapo matibu ya uwingi wao, yatayumbisha uchumi kimatibabu.

Waliongeza, ni kweli akili ni nywele kila mtu ana zake, lakini akili za kuharibu uchumi kwa mabomu, na baadaye kuanza kuhangaikia tiba ya magonjwa yatakayosababishwa na vuruguru za tamaa ya baadhi ya watawala kung’ang’ania madaraka iletayo adha ya kuutweza uchumi, Ipo mlangoni.

No comments:

Post a Comment