Saturday, June 22, 2013

Timu nane kushiriki bonanza la Breake Point Jumapili


JUMLA ya timu nane zimethibitisha kushriki katika bonaza la soka klabu ya Break Point lililopangwa kufanyika Jumapili Juni 23 kwenye viwanja vya Survey (Chuo Kikuu cha Ardhi).
Mkurugenzi wa Breake Point Outdoor Distributors, Daudi Machumu alizitaja timu ambazo ambazo zitashiriki katika bonanza hilo lililodhaminiwa na kampuni ya bia ya Seregeti (SBL) kuwa ni, Rose Garden, Survey, Mbezi Beach na Boko Veterans.
Machumu alisema kuwa timu nyingine ni Clouds Media Group, Magogoni, Umoja na waaandaaji, Break Point ambayo itakuwa chini ya Rodrick “Neymar” Mwambene. Alisema kuwa bonanza hilo  limepangwa kuanza saa 2.30 asubuhi na madhumuni yake ni kuwakutanisha wadau wa michezo na kubadilishana mawazo.
“Lengo kubwa ni kupromoti michezo na kujadili mambo mbali mbali, kampuni ya Break Point Outdoor Distributors ni wadau wakubwa wa michezo na sanaa, tumedhamini mashindano ya urembo na shughuli nyingine, bonanza hili ni fursa pekee kwa wadau kukutana na kustarehe kwa pamoja huku wakipata vinywaji ambavyo vitauzwa kwa bei ya promotion na nyama choma,” alisema Machumu.
Alisema kuwa pia kutakuwa na bia za bure kwa timu shiriki na kuwataka kuzingatia muda kwani wachezaji wa Ligi Kuu na Ligi nyingine hawaruhusiwi na usimamizi utakuwa mkali. “Hii ni fursa kwa wachezaji walioachana na mpira wa miguu wa ushindani, tunataka timu kuzingatia hayo,” alisema.
Machumu alisema kuwa wameandaa burudani mbali mbali ili kunogesha siku hiyo muhimu sana kwa wadau wa michezo. “ Natoa wito kwa mashabiki kufika na timu kuzingatia muda, kwani mtindo utakaotumika utakuwa wa ligi,” alisema.

No comments:

Post a Comment