Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Netiboli ya waandishi wa habari nchini ‘Taswa Queens’ juzi
iliendeleza makali yake ya kutofungwa baada ya kuwagaragaza walimu wa shule ya
Mkuranga katika ziara ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Jahazi la magori la Taswa Queen lilinogeshwa na Mshambuliaji hatari
Sharifa Mustapha wa Majira akisaidiana na Kiungo mchezeshaji ambaye pia ni nahodha
wao timu hiyo Oliver Alobogast wa Mwananchi na kuukaribisha vyema Mwenzi huo kwa kuwafunga walimu hao magoli 38-9.
Kikosi hicho kinachonolewa na Zainabu Ramadhani na Amina Musa
kilianza kilijikuta kikishangiliwa kwa hali ya juu na Mashabiki wa timu ya
Walimu kutokana na mpira safi waliouonyesha dimbani na kipindi cha kwanza
kuongoza kwa magoli 20-2.
Ushindi huo wa awali uliwafanya wachezaji hao kuongeza juhudi ambapo
mpaka mwamuzi anamaliza mchezo huo Taswa Queens iliibuka kidedea kwa magoli
38-9.
Kikosi cha Taswa Queen kilichofanikisha ushindi huo ni pamoja na Sharifa
Mustapha (GA), Zainabu Ramadhani (GS), Farida Husseni(GD),Charity James(GK),
Zuhura Abdunoor(WD), Clezencia Tryphone(WA) na Olver Alobogast(C) huku
Elizabeth John na Zaituni Kibwana wakianzia bechi.
Mbali ya Taswa Queens kuibuka na ushindi huo mfululizo kwa upande wa Taswa
FC, wao bundi anazidi kutanda katika kikosi chake mara baada ya kukubali
kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Wanaume wa Walimu hao licha ya mpambano
kutomalizika mara baada ya kutokea kwa sintofahamu baada ya mchezaji wa Taswa
Zahoro Mlanzi kutoka Jamboleo akizichapa kavukavu na mmoja wa wachezaji wa timu
pinzani kwa madai ya kumchezea rafu za mara kwa mara na kusababisha mwamuzi
kumaliza mpambano zikiwa zimesalia kama dakika 10 kipindi cha pili.
Mwenyekiti wa timu hiyo Majuto Omari alisema, vijana wake walistaili
kushinda mpambano huo na kudai kuwa kuvunjika kwa pambano ndo sababu ya matokeo
hayo.
No comments:
Post a Comment