Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania Teddy Mapunda akiwagawia soda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe za sikuku ya Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana. Wafanyakazi wa kampuni hiyo walisherehekea sikuu hiyo na wanafunzi hao ili kuonyesha upendo.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daud Nasibu akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama inayomilikiwa na taasisi hiyo wakati wa sherehe za Eid Mubarak ziliyofanyika shuleni hapo jana.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam wakiwahudumia chakula cha mchana wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliamua
kusherehekea sikukuu ya Eid Mubarak na wanafunzi hao jana ili kuonyesha upendo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakila chakula cha mchana kilichoandaliwa
na kampuni ya Montage Tanzania wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakicheza mziki aina ya Kwaito jana
wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo
******************************************************
Na Anna Nkinda - Maelezo
Watanzania
wametakiwa kujenga tabia ya kuwajali watu wenye mahitaji maalum ikiwa
ni pamoja na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ili
nao wajione kana kwamba wana wazazi ingawa baadhi yao wamefiwa na wazazi
wao.
Wito
huo umetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage
Tanzania Teddy Mapunda wakati wa sherehe za sikuku ya Eid
Mubarak zilizofanyika katika Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao
ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama
iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Mapunda
alisema ingawa watoto hao hawana wazazi lakini kama jamii itawajali na
kuwaonyesha upendo hawatahisi tofauti ya kutokuwepo kwa wazazi wao kwani
kutakuwa na watu wanaowajali kama vile wazazi wao wako hai.
Mkurugenzi
huyo pia aliipongeza shule hiyo kwa kuzisaidia shule za jirani za
Sekondari za Mahege na Nyamisati ingawa nao wanapata msaada kutoka kwa
wafadhili kwa kuimarisha miundombinu ikiwa ni pamoja na kujenga majengo,
kutoa vitabu, kuweka umeme wa jua na kuwapatia walimu wa mazoezi ambao
wakimaliza vipindi vya kufundisha katika shule ya WAMA-Nakayama wanaenda
kufundisha katika shule hizo.
Naye Kaimu
Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Suma Mensah alisema kuwa shule yake
inawanafunzi 322 wa kidato cha kwanza hadi cha nne kutoka mikoa yote ya
Tanzania ambao ni watoto yatima na wanaoishi katika mazingira
hatarishi.
Kwa
upande wa michezo alisema kuwa wanashiriki michezo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na mpira wa miguu kwa wanawake na mpira wa mikono kwa wanawake ,
drama na riadha.
Aliongeza kuwa
eneo la viwanja wanalo kubwa na la kutosha lakini hawana viwanja rasmi
pia wanakabiliwa na upungufu wa vifaa vya michezo kama vile jezi, viatu
na mipira.
“Kwa
mara ya kwanza shule yetu ilishiriki mashindano ya UMISETA mwaka 2012
na kufikia ngazi ya mkoa hali ambayo imetutia moyo na tunaamini kuwa
ipo siku wanafunzi wetu watafika ngazi ya Taifa”, alisema Mwalimu Mensah
.
Wafanyakazi
wa kampuni ya Montage Tanzania waliamua kusherehekea sikukuu ya Eid
Mubarak na wanafunzi hao ili kuonyesha kuwa wanawajali na kuwathamini.
Pia waliwapatia zawadi za jezi nne za michezo mbili za mpira wa miguu
na mbili za mpira wa mikono na mipira 10, mitano ya mpira wa miguu na
mitano ya mpira wa mikono .
No comments:
Post a Comment