Malkia
wa Zouk nchini Hafsa Kazinja, akiwa na Omari Mkali (kushoto) wakati
wakirekodi wimbo wa 'NIMUOKOE NANI' katika Studio za OM Productions
jijini Dar es salaam wikiendi hii.
*****************************************************
Baada
ya ukimya wa muda mrefu, Malkia wa Zouk Tanzania, Hafsa Kazinja,
anaibuka upya katika fani akiwa na ingizo lake la kwanza kati ya kumi
aliyoandaa kwa kuimba wimbo maarufu wa NUTA Jazz Band uitwao “NIMUOKOE
NANI” anauouleta hewani katika mahadhi ya Zouk.
Hafsa
Kazinja anasema ameamua kurudi ulingoni kwa kutoa wimbo huo ili
kumuenzi Mzee Muhidin Maalim Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani ya
muziki baada ya kufanya kazi hiyo akiwa na bendi mbalimbali tokea mwaka
wa 1960.
“Nimeamua
kuimba wimbo huu wa “NIMUOKOE NANI” ili kumuenzi gwiji huyu wa muziki
kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo naibuka upya baada ya kukaa
kimya kwa muda”, anasema Hafsa ambaye alitoka kwa wimbo wake wa “PRESHA”
aliomshirikisha Banana Zorro.
Hafsa
ameandaa wimbo huo wa “NIMUOKOE NANI” katika studio za OM Productions
ya jijini Dar es salaam chini ya wanamuziki nguli, Abdul Salvador na
Omari Mkali.
“Nafurahi
kwamba wimbo wa NIMUOKOE NANI nimeuimba baada ya kupata Baraka zote
toka kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe.
“Haikuwa
rahisi kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya kwenda kumuona nyumbani
kwake alinifanyisha mtihani wa kuuimba wote kabla ya kuridhika maana
alisema asingefurahi kuona wimbo wake unaimbwa hovyo hovyo na kuharibiwa
radha yake”, anasema Hafsa, ambaye hivi sana anamalizia ngoma zake
zingine tisa alizotunga mwenyewe, kabla ya kuvamia anga kwa mara ingine.
Hafsa
anasema katika ukimya wake amekuwa akifanya utafiti na kujifunza kwa
undani zaidi fani ya muziki, akipata mawaidha maridhawa toka kwa
wanamuziki nguli ndani nan je ya nchi wakiwemo Muhidin Maalim Gurumo,
Omar Mkali, Abdul Salvador na Lokassa ya Mbongo wa Congo aliyekutana na
kufanya naye kazi alipokuwa ziarani Marekani hivi karibuni.
Msanii
huyu wa kizazi kipya anasema ataitambulisha rasmi ngoma ya “NIMUOKOE
NANI” katika tamasha la kumuenzi Mzee Gurumo lililopangwa kufanyika
OKtoba 1, 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
“Natumaini
wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye tamasha hilo name naahidi
kuitendea haki ngoma ya “NIMUOKOE NANI” hivyo wasikose kuja kujionea
wenyewe jinsi sie wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya kazi na wakubwa
wetu wa kazi, anaongezea Hafsa ambaye pia anaandaa video yake pamoja na
ya ngoma zake zingine mpya.
Mkongwe
Abdul Salvador, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa bendi ya TANCUT
ALMASI YA Iringa iliyotamba na mtindo wake wa “FIMBO LUGODA”, anamtaja
Hafsa kazinja mmoja wa wanamuziki wa kike waliojaaliwa sauti nzuri na
kipaji cha hali ya juu hapa nchini.
“Kwa
kuweza kuimba wimbo wa Mzee Gurumo na kupatia kisawasawa inadhihirisha
kwamba Hafsa ni mwanamuziki aliyekomaa maana si mchezo kuimba nyimbo ya
wakongwe kwa ufasaha kama alivyofanya Hafsa.
“Na
hii inadhihirisha kwamba uwezekano wa kizazi kipya na cha zamani
kufanya kazi pamoja ni mkubwa sana na sioni kwa nini isiwe hivyo”,
anasema Salvador.
Omari
Mkali, aliyetamba na bendi ya CHUCHU SOUNDS, chini ya marehemu Yusuf
Chuchu, naye anamwelezea Hafsa Kazinja kama moja ya majembe ya muziki
hapa nchini kwa upande wa kinamama, na kwamba anaweza kufika mbali
endapo kama moto aliokuja nao upya atauendeleza.
No comments:
Post a Comment