ILE video ambayo ilikua inasubiliwa kwa hamu na wadau wa muziki wa kizazi kipya nchini, ‘Bila kukunja goti’ ambayo imeimbwa na wakali wa muziki huo, Ambwene Yesaya ‘AY’ na Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’ tayari imesambazwa katika vituo mbalimbali vya televisheni nchini Afrika Kusini.
Video ya wimbo huo tayari imeanza kuonekana
katika vituo vya Trace, Mtv Base, Channel O na Saund City.
Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, Wimbo huo
umeanza kuonekana katika vituo vya Afrika Kusini na baadae kusambazwa katika
vituo mbalimbali katika nchi tofauti.
Wasanii hao waliondoka nchini katikati ya mwezi
huu kwaajili ya kufanya video ya wimbo huo ambao wadau mbalimbali wa muziki
nchini wanaisubili kwa hamu kutokana na maneno ambayo yametawala katika wimbo
huo.
Mbali na kwenda kurekodi video ya kazi hiyo, wasanii
hao wameamua kuungana tena na kutengeneza nyimbo zingine zaidi ya mbili ambazo
pia wanatarajia kuzisambaza hivi karibuni.
Wasanii hao ni kati ya wasanii wa bongo fleva
nchini wanaofanya vizuri kutokana na kazi zao kukubalika katika tasnia ya
muziki huo ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment