Thursday, October 31, 2013

DIWANI AIPIGA TAFU TIMU YA SOKA YA UHURU FM


 Diwani wa Kata ya Msongola, Ukonga, Dar es Salaam, Angel Malembeka (kulia) ameipiga tafu timu ya soka ya Uhuru FM, kwa kuipatia jozi mbili za jezi na mipira miwili ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano baina ya timu hiyo na kata yake. Pichani, Diwani huyo akikabidhi vifaa kwa uongozi wa timu hiyo, Angel Alikimali na Furaha Luhende, katika hafla fupi iliyofanyika nje ya Jengo la CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo. Wakati Luhende ni Mwenyekiti wa timu hiyo,  Akilimali ambaye ni Kaimu Mkurugebzi Mtendaji wa Uhuru FM ni mlezi wa timu hiyo.
 Akilimali akimshukuru Masala Mabula ambaye ni mchezaji aliyeibuliwa kipaji chake katika michuano ya Malembeka Cup iliyomalizika hivi karibuni ambaye sasa anajiandaa kwenda Msumbiji kucheza soka la kulipwa. Masala alifuatrana na Diwani huyo (kulia)
Luhende na Akilimali wakifurahia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na diwani
 Diwani na Akilimali wakiwa na baadhi ya waandishi na watangazaji wa Uhuru baada ya makabidhiano hayo.
Mtangazaji wa Uhuru FM, Mhina Dungumalo akimhoji diwani huyo baada ya makabidhiano Imetayarishwa na theNkoromo Blog

NBC yawakumbuka watoto wenye mahitaji wa Kituo cha Kurasini


Msaidizi wa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NBC,  Jolanda Songoro (kulia) akishikana mikono na Mkuu wa Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini, Ramadhan Yahya wakati akimkabidhi msaada wa magodoro, vyandarua, vyakula na sabuni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shs milioni 2.5 viliyotolewa na benki hiyo kituoni hapo, jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NBC,  Jolanda Songoro (kushoto) akishikana mikono na baadhi ya watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini, wakati akikabidhi msaada wa magodoro, vyandarua, vyakula na sabuni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shs milioni 2.5 viliyotolewa na benki hiyo kituoni hapo, jijini Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni Meneja Mahusiano wa Benki hiyo, Eddie Mhina.
Msaidizi wa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NBC,  Jolanda Songoro (kushoto) na Meneja Mahusiano wa Benki hiyo, Eddie Mhina wakibeba baadhi ya watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini, wakati benki hiyo ikikabidhi msaada wa magodoro, vyandarua, vyakula na sabuni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shs milioni 2.5 kituoni hapo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni motto, Sebastian na kulia ni Alex.
Mfanyakazi katika Idara ya Fedha ya NBC, Gabriela Sukums (kushoto) na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina (kulia) wakigawa juisi kwa baadhi ya watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini, wakati benki hiyo ikikabidhi msaada wa magodoro, vyandarua, vyakula na sabuni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shs milioni 2.5 kituoni hapo, jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NBC,  Jolanda Songoro (kushoto) akicheza mchezo wa kuruka kamba na baadhi ya watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini.

MWANAMITINDO WA KIMATAIFA MTANZANIA MAGESSE AZIDI KUTESA


 Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka Tanzania, Millen Magesa wakipita jukwaani   kuonesha  mavazi yake katika Tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week, lililofanyika kwenye Stesheni ya Treni ya Ravos ya Mjini Tshwane, Pretoria, Afrika Kusini hivi karibuni.
Mbunifu wa mavazi wa kimataifa nchini Afrika Kusini, David Tlale akiwa na Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka Tanzania, Millen Magesa wakipita jukwaani  stejini mara baada ya kuonesha ya kuonesha  mavazi yake katika Tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week, lililofanyika kwenye Stehsni ya Treni ya Ravos ya Mjini Tshwane, Pretoria, Afrika Kusini hivi karibuni

TIMBULO AIPIKA 'BADO INATAMBA'




Na Elizabeth John


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Timbulo ‘Timbulo’, amewaomba mashabiki wa muziki wa kizazi kipya nchini, wajiandae kupokea kibao chake kipya kinachokuja kwa jina la ‘Bado Inatamba’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Timbulo alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, ambacho anaamini kitakuwa gumzo mtaani kutokana na ujumbe uliopo.

Alisema wimbo huo utakuwa ni changamoto kwa wasanii wenzake, kutokana na baadhi ya ujumbe uliopo ndani ya wimbo huo unaowaonya wasanii kuwa na nyimbo zenye manufaa kwa jamii.

“Kiukweli wasanii wengi wa bongo fleva, tumekuwa tukipeleka mawazo yetu kwenye mapenzi pekee, mimi nimeona kuondoka kwenye mapenzi na kufanya kazi ambazo zinaelimisha jamii kwa kiasi kikubwa,” alisema Timbulo.

Licha ya kutaka kutoka na kibao hicho, Timbulo alishawahi kutamba na vibao vyake kama, ‘Samson na Delila’, ‘Timbulo wa leo’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya

PHD AOMBA RADHI MASHABIKI




Na Elizabeth John
MSANII wa filamu na bongo fleva nchini, Hemed Suleiman ‘PHD’ amewaomba radhi mashabiki wa muziki wake kwa kutoonekana msanii, Heri Samir ‘Mr Blue’ katika video ya wimbo wake wa ‘Rest Of My Life’.
Katika video ya wimbo huo, sauti ya Mr Blue unasika lakini yeye haonekani kitu ambacho kimewashangaza mashabiki wa msanii huyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Hemed alisema hiyo imetokana na msanii huyo kutokuwepo nchini wakati akifanya ‘shooting’ ya wimbo huo.
“Naomba sana radhi kwa mashabiki wangu kwa kutoonekana Mr Blue katika video ya wimbo huo, wakati nafanya video ya wimbo huo, hakuwepo nchini baada ya kuona audio imekaa kwa muda bila video nikalazimika kuifanya pekeyangu,” alisema.

Msanii huyo alishawahi kutamba na kazi zake kama, ‘Mama Kimbo’, ‘Usiniache’, ‘Ninachotaka’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

PHD AOMBA RADHI MASHABIKI




Na Elizabeth John
MSANII wa filamu na bongo fleva nchini, Hemed Suleiman ‘PHD’ amewaomba radhi mashabiki wa muziki wake kwa kutoonekana msanii, Heri Samir ‘Mr Blue’ katika video ya wimbo wake wa ‘Rest Of My Life’.
Katika video ya wimbo huo, sauti ya Mr Blue unasika lakini yeye haonekani kitu ambacho kimewashangaza mashabiki wa msanii huyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Hemed alisema hiyo imetokana na msanii huyo kutokuwepo nchini wakati akifanya ‘shooting’ ya wimbo huo.
“Naomba sana radhi kwa mashabiki wangu kwa kutoonekana Mr Blue katika video ya wimbo huo, wakati nafanya video ya wimbo huo, hakuwepo nchini baada ya kuona audio imekaa kwa muda bila video nikalazimika kuifanya pekeyangu,” alisema.

Msanii huyo alishawahi kutamba na kazi zake kama, ‘Mama Kimbo’, ‘Usiniache’, ‘Ninachotaka’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

ROMA ATANBULISHA VIDEO YA '2030' KESHO


Na Elizabeth John


ILE video ya wimbo unaojulikana kama ‘2030’ iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki wa hip hop nchini, ulioimbwa na mkali wa muziki huo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ inatarajiwa kuzinduliwa Novemba Mosi.
Kwa mujibu wa msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Facebook, alisema mashabiki wa muziki huo wakae mkao wa kula kuipokea video ya wimbo huo ambao upo sokoni tangu Januari mwaka huu.
“Mashabiki wangu wameisubiri kazi hii kwa siku nyingi sana naomba wakae mkao wa kula kuipokea kazi hii ambayo naamini itakuja kuliiteka soko la muziki huo kutokana na maudhui ya wimbo huo,” alisema.
Alisema anatarajia kuanza kuisambaza katika vituo mbalimbali vya televisheni, Ijumaa ya wiki hii hivyo mashabiki wake wasubili kuona kilichozungumzwa katika wimbo huo.

Roma ni kati ya wasanii wa hip hop Tanzania ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo kutokana na mashairi ya nyimbo zake kusimama na kuwa na ujumbe mzito katika jamii inayomzunguka.

AIRTEL MONEY HAKATWI MTU INAWAPIGA TAFU WAFANYA BIADHARA YA SAMAKI MWALONI MUSOMA NA MWANZA.


 kushoto ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na kulia ni Ofisa
Masoko wa kanda ya ziwa Bw Ally Mashauri wakimkabidhi vitendea kazi
vya uwakala Bw, Innocent Godwin (kati) anaefanya uwakala ndani ya soko
la samaki la kimataifa Mwaloni Kirumba Mwanza leo wakati ambapo airtel
walitembelea sokoni hapo kujionea jinsi wauzaji na wanunuzi wa samaki
wanavyoitumia huduma yao ya  kutuma na kutoa pesa bila makato
wanapokuwa kwenye biashara zao-hakatwi mtu hapa
 Wakwanza mbele kushoto ni Meneja uhusiano wa Airtel jacksonm Mmbando
na ofisa masoko wa Airtel Mwanza Bw Ally Mashauri wakimsikiliza bw,
Rashid Moshi mmoja wa wauzaji na mvuvi wa samaki katika soko la
kimataifa la Samaki Mwaloni Kirumba Mwanza leo wakati ambapo Airtel
walitembelea sokoni hapo na kuzungumza na wateja wao jinsi huduma ya
Airtel Hakatwi mtu inavyowafaidisha kufanya biashara zao za kuuza na
kununua samaki kupitia airtel money bila makato- Hakatwi mtu hapa.


Biashara ya samaki kwenye Mwalo wa Musoma mkoani Mara na Kirumba
mkoani Mwanza imepata msukumo wa kipekee baada ya kuanzishwa kwa
kampeni ya hakatwi mtu, ambayo inawawezesha watumiaji wa mtandao wa
airtel kutuma na kupokea pesa bila makato.

Ikiwa inaingia katika mwezi wa tatu sasa kampeni ya hakatwi mtu
inayowawezesha wateja wa airtel money kufanya miamala yao bila makato,
wafanyabiashara na wachuuzi kwenye soko la samaki la Mara Mmusoma
wanatumia kampeni hiyo kama njia ya kupunguza kutembea na pesa muda
wote kwa ajili ya kununua ama kuuza samaki na dagaa

mwenyekiti wa soko la samaki na dagaa mwaloni Musoma Mara bw, Gideon
Dogori anasema airtel money hakatwi mtu ni sawa na kufanya biashara ya
malipo kamili yaani cash kutokana na falsafa yake ya hakatwi mtu.

Anasema wafanyabiashara sokoni hapo hufanya malipo kwa kutumia airtel
money na hawana tena ulazima wa kutembea na maburungutu ya fedha kwa
ajili ya kununulia dagaa ama samaki.

"Tangia hawa jamaa wa airtel waanzishe hii huduma yao ya hakatwi mtu
wafanyabiashara hapa wamekua hawatembei na lundo la hela kama
ilivyokua mwanzoni bali sasa wanauza na kununua bidhaa kwa kutumia
simu zao za mkononi",alisema Bw. Dogori.

"Kuna wengine wanaishi nje ya Musoma kwahiyo wanatuma tu pesa na
wanatumiwa bidhaa zao huko walipo bila kufika hapa sokoni kwasababu
huduma ya airtel money haina makato yoyote" aliendelea kueleza
mwenyekiti wa mwalo wa samaki na dagaa musoma bw. Dogoli.

Bw Dogori anasema faida kubwa inaonekana kwenye huduma hii hasa kuokoa
muda kwa wafanyabiashara, ambapo hawahitajiki kusafiri mwendo mrefu
kwenda sokoni hapo kufanya manunuzi kama ilivyokuwa zamani bali
wanatuma tu hela na kusubiria bidhaa zao huko walipo.

"Huduma hii ingekuwa ya kudumu ingesaidia sana wafanyabiashara kwani
ka muda huu mfupi imeweza kusaidia kuongeza hata miataji kwa
wafanaybiashara hapa mwaloni", alisisitiz Dogori.

Bi Mkami Magesa ni mfanyabiashara kwa zaidi ya miaka kumi sokoni hapo,
anasema wakati huu biashara imerahisishwa sana kwani kupitia huduma ya
hakatwi mtu amekuwa akifanyabiashara kubwa na anapata pesa yake bila
makato.

"Hii huduma ya airtel money ya hakatwi mtu ni mkombozi kwakweli kwani
mteja anaweza akawa shinyanga ama singida anatuma humu pesa na mimi
nampakilia mzigo wake anaupata bila ya yeye kufika hapa mwalini",
alisema bi Mkami.

Kwa upande wake John Anton  mchuuzi wa dagaa na samaki katika  soko la
samaki Mwaloni Mwanza Anasema anachofanya ni kutoa oda ya bidhaa
anazohitaji na kisha kutuma pesa bila makato kwenda kwa muuzaji na
kuokoa muda wa kusafiri kutoka sirali anapoishi na kufanyia biashara
zake.

"Kwasasa maisha na biashara imekuwa rahisi sana nawaomba airtel
kuifanay huduma hii kuwa endelevu maana inasaidia sana katika shughuli
za kibiashara", alisema Bw. Bundala.

Bw Dogori ambaye ni mwenyekiti wa mwaloni mjini Musoma alimalizia kwa
kusema elimu zaidi ya matumizi ya huduma za airtel money inahitajika
kwani zimeanza kuonesha dalili za kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wa
soko lake.

TASWA WAPONGEZA UONGOZI MPYA WA TFF


 
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliochaguliwa Jumapili iliyopita.
 
Tunaungana na wapenda michezo na Watanzania kwa ujumla kuitakia kila la heri Kamati ya Utendaji ya TFF na shirikisho hilo kwa ujumla chini ya Rais mpya Jamal Malinzi na Makamu wake, Wallace Karia.
 
TASWA inaamini Malinzi, Karia na wajumbe wao ni wazoefu na ni watu wenye kujua mambo mengi yanayohusu mpira wa miguu nchini, hivyo tunaamini watakuwa viongozi wazuri kwa nafasi zao katika kuhakikisha shirikisho hilo linasonga mbele.
 
Tunawatakia kila la heri Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji, huku tukiamini hawatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliowaamini kushika nafasi hizo.
 
TASWA na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla hapa nchini tunaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili watekeleze majukumu yao ipasavyo.
 
Nawasilisha.
 
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
30/10/2013

DK.Shein atoa salamu za Mwisho Marehemu Balozi Sepetu.


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimpa pole Mjane wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,Mama Miriam Sepetu,alipofika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja,kuuaga mwili wa Marehemu leo Asubuhi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitia saini kitabu cha maombolezo ya Marehemu Balozi Isaac Sepetu,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja leo asubuhi,Marehemu alifariki juzi Jijini Dae es Salaam,na atazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiuwaga Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la

zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja leo asubuhi,Marehemu alifariki juzi Jijini Dae es Salaam,na atazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.
Baadhi ya Wananchi  mbali mbali  wakiwa katika sehemu maalum nje ya  ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja,wakisubiri kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,leo asubuhi ambapo utazikwa  Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}

KAMPUNI YA BRAVO YAWAPATIA KAZI DUBAI WATANZANIA WENGINE WAWILI


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bravo Job Centre, Jaffar Kingwande (kulia), akimkabidhi tiketi Amisa Ally (22), ya kwenda Dubai kufanya kazi ya ndani aliyotafutiwa na kampuni hiyo. Anayeshudia hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Mohamed Omar. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Jazira Rashid akipatiwa tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda Dubai kufanya kazi aliyotafutiwa na kampuni hiyo.

 Amisa na Jazira wakiwa na baadhi ya maofisa wa Bravo pamoja na wadhamini wao
Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Omar akifafanua jambo wakati wa kuwaaga wafanyakazi hao

BABU SEYA NA MWANAYE WAANZA KUSIKILIZWA RUFAA YAO NA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA


 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo. Nguza na Papii walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na ulawiti.





 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.


Nguza Vicking akipunia watu mahakamani

Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.

RAIS WA CAF AMPONGEZA MALINZI


Jamal Malinzi
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.
Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.
Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.
PAMBANO LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.
Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.
Wamiliki wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.
SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Wednesday, October 30, 2013

WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KONYAGI (TDL) WALIOKWENDA KUONA MECHI YA BARCELONA NA REAL MADRID,HISPANIA WAREJEA WAKIWA NA BASHASHA TELE


Mfanyakazi wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Khadija Madawili ambaye alikuwa kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa TDL waliokwenda kushuhudia pambano la Ligi ya La Liga ya Hispania kati ya Barcelona na Rael Madrid, akirejea jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Wafanyakazi watano wa TDL, waliteuliwa baada ya kampuni hiyo kushinda  Tuzo ya SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13)
 Joseph Chibehe (kushoto) akilakiwa na mkewe baada ya kuwasili
                                             Chibehe akiwa na furaha baada ya kulakiwa na mkewe
 Bavon Ndumbati (kushoto), akilakiwa na ndugu yake. Katikati ni Michael Mrema
                                                              Bavon akiwa na furaha
                                                                 Mwesiga Mchuruza.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (katikati), akiwa na mabosi wa kampuni mama ya SABMILLER AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya  MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13).

KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd, (KONYAGI) ambayo ni miongoni mwa kampuni tanzu za Kampuni ya Sabmiller South Africa, imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13). Sabmiller inamiliki zaidi ya viwanda 60 vya bia na vinywaji vingine duniani.

Baada ya ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TDL, Mgwassa ambaye alipambana mpaka kupata ushindi huo, aliamua kuwazawadia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, kwenda Hispania kushuhudia pambano la timu kubwa za Barcelona na Real Madrid lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Wafanyakazi waliokwenda Hispania  na kurejea jana usiku kwa ndege ya Afrika Kusini ni; Joseph Chibehe, Khadija Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesiga Mchuruza.

Wafanyakazi hao, walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, walionekana kuwa na bashaha na kupokelewa na ndugu zao pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzie,Michael Mrema wa Kanda ya Kaskazini, alisema kuwa wanashukuru uongozi kuwapa zawadi hiyo, ambayo imewafanya kuwa na morari mpya wa kazi.

Pia anaseama walifurahi sana kushuhudia mechi hiyo kubwa ya timu za Barcelona na Real Madrid ambapo timu ya Barcelona waliyokuwa wanaishabikia kushinda mabao 2-1.