Thursday, October 17, 2013

KINYOGOLI AMKUMBUKA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE


MWALIMU Julius Kambarage Nyerere kipindi yuko madarakani, alipenda michezo kuanzia mashuleni hadi kwenye makampuni na mashirika mbalimbali hapa nchini, ingawa alikuwa akipenda mchezo wa bao.
Aliweka sera bora ya michezo na kufanikisha kuundwa kwa Baraza la Michezo la Taifa mwaka 1967 na kutoa fursa zaidi kwa wenye vipaji kuvionyesha.
Kwa mujibu wa bondia mahiri wa Ngumi hapa nchini, ambaye kwa sasa ni kocha mongwe wa mchezo wa masumbwi nchini, Habibu Ally Kinyogoli (65), Nyerere alifanikisha wachezaji wa Tanzania kuitangaza zaidi nchi yetu na kufanya vizuri kutokana na mazingira bora yaliyokuwako wakati huo.
Kinyogoli ni mwanachama wa klabu ya  Simba lakini hahudhurii michezo ya timu hiyo, mapenzi yake yanabaki kwenye ngumi.
Nyota yake ya michezo ilianzia shuleni, Manerumango Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, mwaka 1958, alicheza soka, ngumi na riadha, aliendelea na mchezo wa ngumi kwa sababu ndio ulikuwa ndani ya damu yake, michezo mingine ilimshinda kwa sababu ya hasira za baadhi ya wachezaji pindi zinapotokea rafu.
Kinyongoli wakati alipokuwa akicheza, alikuwa pia akitoa mafunzo kwa wenzake, mwaka 1966, katika klabu ya Magomeni Centre yalipo makao Makuu ya Manispaa ya Kinondoni alimfunza Majuto Mahavu ambaye baadae alikuwa tishio kwenye timu ya Taifa.
Mwaka 1970 alijitosa rasmi kwenye ngumi baada ya kuvutiwa na Titus Simba aliyeiletea medali ya kwanza Tanzania ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Scotland, ndipo na yeye akaongeza ufanisi zaidi katika mchezo huo.
Mwaka 1971 aliajiriwa kiwanda cha Bora baada ya kuonesha umahiri katika mchezo huo, akafanikiwa kumfudinsha ngumi, Marehemu Zakaria Yombayomba, mwaka 1973 aliasisi klabu ya ngumi ya Urafiki akawaibua akina Charles Mhilu ‘Spinks’, Habibu Mzungu, Lazaro Makarious, Kwelu Msinjili na wengineo.
Mwaka 1972 alishiriki mashindano ya Olimpiki, Munich Ujerumani walikwenda na akina Titus Simba, Robert Mwakosye, Bakari Suleimani ‘Match Maker’, Said Tambwe katika mashindano hayo, mwanariadha Clever Kamanga aliipa Tanzania medali ya shaba kwa mbio za umbali za mita 400.
Katika mashindano hayo, Kinyogoli alifanya vibaya baada ya kukatika kwa mshipa wa mkono wa kulia katika mazoezi nchini humo, mchezo wa kwanza wa Olimpiki alishinda kwa pointi nyingi dhidi ya Mcambodia, mchezo wa pili alipoteza pambano baada ya kujitonesha mkono wake na damu zikatoka nyingi.
Maumivu hayo hakuyaona hadi, Profesa Philemon Sarungi wakati huo alikuwa akisoma nchini humo, alijitolea kuisaidia timu hiyo.
Mwaka 1973 alishiriki All Africa Games jijini Lagos Nigeria akarejea na medali ya fedha na kuchaguliwa kwenye timu ya Afrika iliyoshiriki Inter-Continental  iliyofanyika Mexico , uteuzi huo pia uliwahusu pia akina Jacob Mussa, Bakari Suleimani, Titus Simba na Mbaraka Mkanga wakati katika soka Tanzania iliwakilishwa na akina Maulid Dilunga, Abdallah Kibadeni na Kitwana Manara.
Mwaka 1974 alisisi klabu ya Simba ambayo kipindi hicho ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti, Abubakar Mwilima baada ya kuchana mkataba wa Bora, baada ya uongozi mpya wa kiwanda hicho kutokupenda michezo, akaondoka na wenzake wote aliokuwa nao kiwandani hapo kama Bakari Suleiman ‘Match Maker’, YombaYomba na wengineo.
1976 akiwa kwenye kambi ya maandalizi ya Olimpiki alitangaza kujiuzulu kuchezea timu ya Taifa, mwaka 1978 akaanzisha klabu za watoto wadogo Simba Sports Klabu  na kuendelea na Relwe Gelezani, Simba wakachipuka akina ukoo wa Matumla Rashid,Haji,ali,hassani,Mazimbo, Mbwana,Karimu Matumla, wote hawo ni wa ukoo mmoja na kina  Iraq Hudu Mkumwena, Remmy Ngabo, Joseph Marwa,Shabani Mhamila 'Star Boy' Iddy Hamisi 'Bowe' Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa ni msaidizi wake katika kuinuwa vijana chipkizi, Mohamed Chipota,Oscar Manyuka na wengineo.
Hivi sasa, Kinyogoli anafundisha klabu ya Amana ya Ilala na akiendelea na Simba pia akiwa na changamoto nyingi ambazo ni uwezeshwaji wake kutoka kwa wadau mbalimbali kwa sababu ameutengeneza mchezo huo tangu alipokuwa akifanya kazi na alitumia gharama zake lakini sasa, kazi hafanyi na wadau wengi wa mchezo huo kuto mkumbuka kwa kutoa sapoti ya aina yoyote hivyo anatoa wito kwa wote pamoja na taifa zima kuwa yeye kwa sasa anapatikana Amana Ilala Dar es salaam 

hivyo anawaomba wadau wamsaidie angalau vifaa vya mchezo ili aweze kuenderea kuwanoa vijana wengi zaidi kama alivyofanya hapo nyuma kwa wanaoitaji kumsaidia kocha huyo wanaweza kumpigia simu 0655928298 au 0756928298 
au zaidi wafike kumuangalia anavyo endelea kuinua vipaji vya vijana wengi kwa sasa pale Amana ukifika uliza MASTER KINYOGOLI kocha wa mchezo wa masumbwi nchini  zaidi unaweza kuwasiliana na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini

Rajabu Mhamila 'Super D'
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

No comments:

Post a Comment