MWALIMU Julius Kambarage Nyerere kipindi yuko madarakani,
alipenda michezo kuanzia mashuleni hadi kwenye makampuni na mashirika
mbalimbali hapa nchini, ingawa alikuwa akipenda mchezo wa bao.
Aliweka sera bora ya michezo na kufanikisha
kuundwa kwa Baraza la Michezo la Taifa mwaka 1967 na kutoa fursa zaidi kwa wenye
vipaji kuvionyesha.
Kwa
mujibu wa bondia mahiri wa Ngumi hapa
nchini, ambaye kwa sasa ni kocha mongwe wa mchezo wa masumbwi nchini,
Habibu Ally Kinyogoli (65), Nyerere alifanikisha wachezaji wa Tanzania
kuitangaza zaidi nchi yetu na kufanya vizuri kutokana na mazingira bora
yaliyokuwako wakati huo.
Kinyogoli ni mwanachama wa klabu ya Simba lakini hahudhurii michezo ya timu hiyo, mapenzi yake
yanabaki kwenye ngumi.
Nyota yake ya michezo ilianzia shuleni,
Manerumango Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, mwaka 1958, alicheza soka, ngumi na
riadha, aliendelea na mchezo wa ngumi kwa sababu ndio ulikuwa ndani ya damu
yake, michezo mingine ilimshinda kwa sababu ya hasira za baadhi ya wachezaji
pindi zinapotokea rafu.
Kinyongoli wakati alipokuwa akicheza, alikuwa
pia akitoa mafunzo kwa wenzake, mwaka 1966, katika klabu ya Magomeni Centre
yalipo makao Makuu ya Manispaa ya Kinondoni alimfunza Majuto Mahavu ambaye
baadae alikuwa tishio kwenye timu ya Taifa.
Mwaka 1970 alijitosa rasmi kwenye ngumi baada ya
kuvutiwa na Titus Simba aliyeiletea medali ya kwanza Tanzania ya Jumuiya ya
Madola iliyofanyika Scotland, ndipo na yeye akaongeza ufanisi zaidi katika
mchezo huo.
Mwaka 1971 aliajiriwa kiwanda cha Bora baada ya
kuonesha umahiri katika mchezo huo, akafanikiwa kumfudinsha ngumi, Marehemu Zakaria
Yombayomba, mwaka 1973 aliasisi klabu ya ngumi ya Urafiki akawaibua akina
Charles Mhilu ‘Spinks’, Habibu Mzungu, Lazaro Makarious, Kwelu Msinjili na
wengineo.
Mwaka 1972 alishiriki mashindano ya Olimpiki,
Munich Ujerumani walikwenda na akina Titus Simba, Robert Mwakosye, Bakari
Suleimani ‘Match Maker’, Said Tambwe katika mashindano hayo, mwanariadha Clever
Kamanga aliipa Tanzania medali ya shaba kwa mbio za umbali za mita 400.
Katika mashindano hayo, Kinyogoli alifanya
vibaya baada ya kukatika kwa mshipa wa mkono wa kulia katika mazoezi nchini
humo, mchezo wa kwanza wa Olimpiki alishinda kwa pointi nyingi dhidi ya
Mcambodia, mchezo wa pili alipoteza pambano baada ya kujitonesha mkono wake na
damu zikatoka nyingi.
Maumivu hayo hakuyaona hadi, Profesa Philemon
Sarungi wakati huo alikuwa akisoma nchini humo, alijitolea kuisaidia timu hiyo.
Mwaka 1973 alishiriki All Africa Games jijini
Lagos Nigeria akarejea na medali ya fedha na kuchaguliwa kwenye timu ya Afrika
iliyoshiriki Inter-Continental
iliyofanyika Mexico , uteuzi huo pia uliwahusu pia akina Jacob Mussa,
Bakari Suleimani, Titus Simba na Mbaraka Mkanga wakati katika soka Tanzania
iliwakilishwa na akina Maulid Dilunga, Abdallah Kibadeni na Kitwana Manara.
Mwaka 1974 alisisi klabu ya Simba ambayo kipindi
hicho ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti, Abubakar Mwilima baada ya kuchana
mkataba wa Bora, baada ya uongozi mpya wa kiwanda hicho kutokupenda michezo,
akaondoka na wenzake wote aliokuwa nao kiwandani hapo kama Bakari Suleiman
‘Match Maker’, YombaYomba na wengineo.
1976 akiwa kwenye kambi ya maandalizi ya
Olimpiki alitangaza kujiuzulu kuchezea timu ya Taifa, mwaka 1978 akaanzisha
klabu za watoto wadogo Simba Sports Klabu na kuendelea na Relwe Gelezani,
Simba wakachipuka akina ukoo wa Matumla
Rashid,Haji,ali,hassani,Mazimbo, Mbwana,Karimu Matumla, wote hawo ni wa
ukoo mmoja na kina Iraq Hudu Mkumwena, Remmy Ngabo, Joseph
Marwa,Shabani Mhamila 'Star Boy' Iddy Hamisi 'Bowe' Rajabu Mhamila
'Super D' ambaye kwa sasa ni msaidizi wake katika kuinuwa vijana
chipkizi, Mohamed Chipota,Oscar Manyuka na wengineo.
Hivi sasa,
Kinyogoli anafundisha klabu ya
Amana ya Ilala na akiendelea na Simba pia akiwa na changamoto nyingi
ambazo
ni uwezeshwaji wake kutoka kwa wadau mbalimbali kwa sababu ameutengeneza
mchezo
huo tangu alipokuwa akifanya kazi na alitumia gharama zake lakini sasa,
kazi
hafanyi na wadau wengi wa mchezo huo kuto mkumbuka kwa kutoa sapoti ya
aina yoyote hivyo anatoa wito kwa wote pamoja na taifa zima kuwa yeye
kwa sasa anapatikana Amana Ilala Dar es salaam hivyo anawaomba wadau wamsaidie angalau vifaa vya mchezo ili aweze kuenderea kuwanoa vijana wengi zaidi kama alivyofanya hapo nyuma kwa wanaoitaji kumsaidia kocha huyo wanaweza kumpigia simu 0655928298 au 0756928298
au zaidi wafike kumuangalia anavyo endelea kuinua vipaji vya vijana wengi kwa sasa pale Amana ukifika uliza MASTER KINYOGOLI kocha wa mchezo wa masumbwi nchini zaidi unaweza kuwasiliana na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini
No comments:
Post a Comment