Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
MABINGWA
wa zamani mara mbili mfululuizo wa ligi kuu Tanzania mnamo mwaka 1999
na 2000, wakata miwa wa mashamba ya Manungu Turiani mkoani Morogoro,
Mtibwa Sugar wametamba kuendeleza vipigo ligi kuu kama walivyofanya
mechi mbili zilizopita kwa lengo la kurejesha heshima yao.
Afisa habari wa klabu hiyo, Tobias Kifaru Lugalambwike imepiga stori na mtandao wa FULLSHANGWE na
kueleza kuwa kipigo walichotoa kwa JKT Oljoro cha mabao 5-2 na 4-1 kwa
Mgambo JKT ni kiashirio cha kurejea mchezoni na sasa mipango ni kufanya
maandalizi ili kuendeleza dozi zaidi kwa timu za ligi kuu.
“Ligi
ya msimu huu imekuwa na ushindani mkubwa, tulianza vibaya na watu
wakajua Mtibwa hawana lolote, salamu zetu!, tulikuwa tunazisoma timu na
imetuchukua muda kidogo kuzijua, sasa tumeshawapikia dawa yao na ndio
maana umeona vipigo hivyo tulivyotoa hapa Manungu”. Alitamba Kifaru.
Afisa
habari huyo alisema miaka ya 1999 na 2000 Mtibwa Sugar ilizishinda
Simba na Yanga na timu nyingine na kubeba kombe, sasa imefika wakati wa
kurejesha heshima yao licha ya kuwepo timu mpya zinazotisha kwa sasa.
“Hizi
timu za Azam fc, Mbeya City hazifikia ubora wa Mtibwa na ukongwe wake,
tumekuwepo kwenye ligi kwa zaidi ya miaka 20, unapozungumzia timu za
ligi kuu zenye historia nzuri unataja Simba, Yanga na Mtibwa, kwa
waliozaliwa miaka ya karibuni hawatutambui makali, tuko ngangari
kinoma”. Alisema Kifaru.
Kifaru
aliongeza kuwa kwa sasa wanajiandaa na mechi ya Octoba 28 mwaka huu
katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga dhidi ya wagosi wa Kaya,
Coastal union, huku lengo lao likiwa ni kuendelea kuzoa pointi tatu
muhimu.
“Kocha
wetu Mecky Mexime anaendelea kunoa wembe wa vijana wetu, Coastal
hawatupi shida sana, tunawaheshimu sana na ikizingatiwa kwa sasa
wanafanya vibaya kwani wamepoteza mechi mbili mfulululizo, lakini kwetu
lazima waje kukubali kipigo tena”. Alisema kifaru.
Coastal
Union walisajili wachezaji wakali lakini siku za hivi karibuni wamekuwa
wakiambulia matokeao mabaya, na mechi mbili zilizopita walifungwa 2-1
na Ashanti United na wikiendi iliyopita wakala 1-0 dhidi ya Kagera Sugar
mjini Bukoba dimba la Kaitaba.
Baadhi
ya nyota waliosajiliwa na Coastal Unioni ni pamoja na Haruna Moshi
`Boban` , Juma Nyoso, Crispine Odula Wadenya, Kata Yayo, Keneth
Masumbuko, na wengineo.
Mtibwa
wao wataingia katika mchezo huo wakichekelea, kwani mechi mbili
zilizopita walimtafuna JKT Oljoro 5-2 na wikiendi iliyopita wakamfumua
Mgambo JKT mabao 4-1.
No comments:
Post a Comment