Baadhi ya vijana wakiwa wamebeba bango lililokuwa na ujumbe uliosema;
“Tutazika mpaka lini Kizuiani?”
“Tutazika mpaka lini Kizuiani?”
………………………………………………………………………..
NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
Wakazi
wa Kizuiani Mbagala jijini Dar es Salaam, jana walizua vurugu na kuziba
kwa muda wa saa mbili barabara ya Kilwa na kusababisha magari mengi
kushindwa kuendelea na safari zao kisa kikiwa Mwanafunzi Adina Seleman
(11) wa darasa la 5 kugongwa na gari aina ya Scania na kufariki papo
hapo.
Tukio
hilo lilitokea saa 5.45 asubuhi wakati mwanafunzi huyo aliyekuwa
akisoma katika Shule ya Msingi Kibondemaji akivuka barabara katika eneo
hilo. Wakazi hao walizusha vurugu hizo ikiwa ni njia ya kuishinikiza
Wakala wa
Baraba nchini, Tanroad kuweka matuta ili kuzuia ajali zinazotokea mara
kwa mara katika eneo hilo.
Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa wa Kizuiani, Mashaka
Selemani, watu 30 wamepoteza maisha kwa ajali katika eneo hilo tangu
barabara hiyo ikamilike mwaka 2009.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo aliyekuwepo katika zoezi la kuwatawanya vijana walioziba barabara hiyo kwa magogo, kuchoma matairi moto na mawe akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha uvunjifu wa sheria.
Maaskari wakiwa katika eneo la tukio. Askari wa Ulinzi Shirikishi wa Mbagala wakimbeba msobemsobe ili kumuingiza ndani ya gari la polisi mmoja wa vijana aliyehisiwa alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakileta vurugu.
No comments:
Post a Comment