Saturday, January 4, 2014

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye:''mwanachama yeyote wa CCM anayetangaza nia ya kuwania nafasi ya urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa, anapoteza sifa ya kuwa mgombea.''


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  

 Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mwanachama yeyote anayetangaza nia ya kuwania nafasi ya urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa, anapoteza sifa ya kuwa mgombea.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema Dar es Salaam jana kwamba chama hicho kinaamini katika umoja na mshikamano na kwamba wanaotangaza nia ya kugombea urais kabla ya muda wamepoteza sifa kwa kuwa ni kama wanakigawa.
 
Juzi, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alitangaza nia ‘kimtindo’ akisema anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumani ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
 
Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitangaza hayo katika ibada ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli.
 
Nape alisema wanaotangaza nia ya kuwania urais hivi sasa wanafahamu kwamba hawana sifa za kuwa wagombea wa nafasi hizo kwa sababu mbalimbali.Kwahabari kamili BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment