Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema Dar es Salaam jana
kwamba chama hicho kinaamini katika umoja na mshikamano na kwamba
wanaotangaza nia ya kugombea urais kabla ya muda wamepoteza sifa kwa
kuwa ni kama wanakigawa.
Juzi,
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alitangaza nia ‘kimtindo’ akisema
anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumani ya ndoto zake, ambayo pia
itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na
maendeleo ya uhakika.
Lowassa
ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais
kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitangaza hayo katika ibada
ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli.
Nape
alisema wanaotangaza nia ya kuwania urais hivi sasa wanafahamu kwamba
hawana sifa za kuwa wagombea wa nafasi hizo kwa sababu
mbalimbali.Kwahabari kamili BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI>>>
No comments:
Post a Comment