Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 25, 2014

WASANII WA FILAMU WAASWA KUACHA KUTUMIA MAJANGA HALISI KUTENGENEZA FILAMU


IMG_9886Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman (kushoto) . akifafanua jambo  kuhusu  filamu  ya  MV spice  Islander. Kulia ni Katibu  Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo.IMG_9914Katibu  Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo(kulia) akifafanua jambo  kuhusu  filamu  ya  MV spice  Islander . Kushoto ni Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman  .IMG_9950Katibu  Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo(kushoto) akipeana mkono na Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu  ya  Steps,  Moses  Mwanyilo (kulia).Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman (kushoto) akipeana mkono  kulia na Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu  ya  Steps,  Moses  Mwanyilo. (Picha na Magreth Kinabo)
………………………………………………………………………………
Na Magreth  Kinabo – Maelezo

 Viongozi  wa Bodi za Filamu  wa Tanzania Bara na Zanzibar wametoa ushauri  kwa wasanii nchini  kuacha kutumia majanga halisi kwa ajili ya kutengenezea filamu Kibiashara.

Kauli hiyo imetolewa jana na viongozi  hao , wakati wa kikao cha  kati ya  Katibu  Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo  na  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman  na Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu ya Steps,  Moses  Mwanyilo  kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

 Akizungumza katika kikao hicho, Bi.Fissoo   alisema  kampuni hiyo imetengeneza  filamu  ya  MV Spice  Islander kwa  kuchukua picha halisi za ajali ya  MV spice,ambayo iliwasilishwa katika ofisi yake Novemba 2013 kitendo ambacho ni kinyume na sheria , taratibu na kanuni  za utengenezaji wa filamu.

Alisema filamu hiyo ilichukua picha halisi ya ajali hiyo, hivyo ofisi yake ilimwandikia barua mtengenezaji huyo kuwa ibadilishwe, lakini aliomba ashiriki kikao na bodi. Hata hivyo aliitwa mara nne kwa ajili ya kikao na bodi hiyo  lakini hakushiriki  badala yake alileta marekebisho ya  filamu hiyo mara tano ambayo bado yalikuwa na kasoro hizo.

 Naye Bw. Suleiman    alisema filamu hiyo ni muhimu . Hivyo alimtaka mtengenezaji huyo kutoingilia uhuru wa mtu, jamii na Serikali na kutaka filamu hiyo ifanyiwe marekebisho, hivyo ni vema wasanii wakawa wabunifu kutengeneza  filamu zinazogusa  bila kutumia  uhalisia wa janga na majina halisi.   

Aliipongeza bodi ya filamu  ya Bara kwa ushirikiano waliouonesha kwa kuwa filamu ikikataliwa Zanzibar na Bara inakataliwa kwani  kazi kama hiyo iliwasilishwa Zanzibar na ilikataliwa kwa kuwa ajali iliyotokea si sherehe, bali itatonesha  vidonda vya watu walioathirika.

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni hiyo alikiri kosa hilo na aliahidi kufanya marekebisho katika filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...