|
Mgeni
Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro
(kushoto), huku akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake
wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, Happy John wakikata keki
kuashiria uzinduzi rasmi wa kikundi hicho, katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel
iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania
(SWAUTA), kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili
kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba). Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Divas. |
|
Mgeni
Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro (wa
pili kulia), akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha
Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA ) cha Kinondoni, kabla
ya kuzindua rasmi Kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania
‘Airtel Divas’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza
bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao
lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Kushoto ni mwanachama wa Swauta, Adelina Mluge. |
|
Wanachama
wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,
wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na kikundi cha Sauti ya Wanawake
wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa Airtel Divas, uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza bidhaa
zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo
katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). |
|
Ni bidhaa zilizotengenezwa na kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni. |
|
Mgeni
rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro
(kushoto), akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde
(kulia), baada ya kutembelea bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha
Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kabla
ya kuzindua rasmi Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania
‘Airtel Divas’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza
bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao
lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). |
|
Wanachama
wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,
wakilisakata rhumba, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kikundi hicho,
uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo,
Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu
Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na
kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa
Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). |
|
Wanachama
wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,
wakilisakata rhumba, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kikundi hicho,
uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo,
Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu
Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na
kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa
Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). |
|
Mgeni
Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro,
akifurahia zawadi ya kitenge baada ya kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi
wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba (kulia), katika hafla ya
uzinduzi rasmi wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania
‘Airtel Divas’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya
Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kuuza bidhaa zao
kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo
katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). |
|
Picha ya pamoja na kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni. |
Press Release
Airtel Divas watoa msaada kwa wanawake wasiojiweza
Umoja wa wafanyakazi wanawake wa Airtel ujulikanao kama Airtel Divas
umejitoa kuwasaidia na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu
Tanzania (SWAUTA ) kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi hao wa Airtel walifanya uzinduzi rasmi wa Airtel Divas na
kualika kikundi cha SWAUTA kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wafanyakazi
wa Airtel na kuwawezesha kupata fedha kwaajili ya kuwa na banda lao
katika maonyesho ya 38 ya kimataifa ya SABASABA.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Meneja Rasilimali watu Sophia Melamali
alisema” tunayofuraha kuzindua rasmi Airtel Divas mpango maalumu wenye
lengo la kuwainua na kuwahamasisha wanawake na wafanyakazi wa Airtel
kuzifikia ndoto zao.
Kama tunavyofahamu wanawake wanayo majukumu makubwa ya familia na kazi,
hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kugawa muda wao kwa ufanisi. kwa
kupitia Airtel Divas tunashirikiana kwa pamoja kupeana ujuzi na mawazo
ya namna ya kupambana na changamoto hizi na kufikia mafanikio katika
malengo tuliyojiwekea.
Sambamba na hilo tunawahamasisha wanawake kushiriki katika kujitolea na
kutoa msaada kwa jamii na ndo maana leo tumewaalika kina mama hawa wenye
ulemavu na kuwapa nafasi ya kuuza bidhaa zao na kiasi cha pesa
watakachopata leo tutakiongeza mara mbili na kuwawezesha kupata fedha za
kutosha kulipia banda katika maonyesho ya sabasaba. Tunaamini kwa
kufanya hivi tutawawezesha kukuza biashara yao. Natoa wito kwa
watanzania watakaopata nafasi ya kwenda kwenye maonyesho haya wapate
nafasi ya kuwatembelea na kuwaaunga mkono pia.
Akiongea mara baada ya kukabithia msaada huo mwenyekiti Kikundi cha
Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania SWAUTA bi Stella Jairosi
Alisema, Tunawashukuru Airtel kwa kutuwezesha kupata banda zuri liliopo
eneo zuri katika maonyesho ya Sabsaba, kwa miaka 8 sasa tumekuwa
tukishiriki katika maonyesho haya lakini hatukuwahi kuwa na banda letu
wenyewe. Kupitia msaada huu kutoka Airtel kutatupatia mwanya wa
kuonyesha bidhaa zetu na kupata mwaya wa kuuza kwa soko la ndani na la
nje na pia kutatusaidia kuuza bidhaa zetu kwa kiasi kikubwa na kuongeza
pato letu na hivyo kuendeleza miradi ambayo hatukuweza kuifanya kutokana
na uhaba wa fedha.
Kwa upande wake mgeni rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro alisema“
nimejisikia furaha kuwa mgeni rasmi katika shughuli ya leo na napenda
kuwapongeza sana Airtel Divas kwa kujitolea kusaidia jamii kupitia
shughuli hizi za huduma kwa jamii wakiwemo wa mama hawa wa kikundi cha
walemavu nawahamasisha muendelee na juhudi hizi.Pamoja na hayo pia
nachukua nafais hii kuwahimisha Airtel Divas kufanya kazi kwa bidii na
kuonyesha uwezo wao katika maeneo yao ya kazi ili waweze kupata nafasi
nyeti katika Uongozi
No comments:
Post a Comment