Thursday, June 19, 2014

WANAFUNZI DAR WAVUTIWA NA SHUGHULI ZA NISHATI NA MADINI

 Kamishna Msaidizi wa Madini, Uratibu, Mhandisi John Shija  akiwaeleza  wanafunzi  namna shughuli za  uchimbaji madini zinavyofanyika nchini  wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini katika Maonesho  ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja , Jijini Dar es Salaam 

  Mtaalamu wa madini ya Vito vya Rangi na Almas Bibi Teddy Goliama kutoka Kitengo cha Uthamini Madini ya Almas na Vito (TANSORT), Wizara ya Nishati na Madini, akiwaeleza wanafunzi kuhusu aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara.  Anayesikiliza wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Uratibu, Mhandisi John Shija.
Mhandisi  Mwandamizi  Masoko na Huduma kwa Wateja, Juliana Pallangyo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) akitoa ufafanuzi kuhusu namna Shirika hilo linavyofanya kazi kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Taasisi hiyo.
1.  Afisa Habari kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Yisambi Shiwa, akiwaonesha baadhi ya madini yanayopatikana nchini wanafunzi waliotembelea banda la TMAA.
========  =======
Wanafunzi Dar es Salaam Wavutiwa na Shughuli za Nishati na Madini
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Baadhi ya Wanafunzi kutoka baadhi ya Shule za Sekondari mbalimbali Jijini Dar es Salaam wametembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini yake kutaka kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na zinazofanyika.

Wakati wanafunzi hao walipotembelea Wizara na Taasisi zake, wameoneshwa kuvutiwa na kutaka kufahamu kuhusu namna shughuli za uchimbaji madini nchini zinavyofanyika, kutaka kufahamu aina za madini yenye thamani kubwa na  madini yenye uzito mkubwa.

Vilevile, wanafunzi hao wametaka kuelimishwa kuhusu shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi zinazofanyika nchini ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu vyuo mbalimbali vinavyotoa mafunzo kuhusu masuala ya gesi, mafuta na madini.

Aidha, wengi wao walipenda kuona madini ghafi ya Tanzanite yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na kufahamu aina zote za madini yaliyopo chini. Wanafunzi hao wamepata nafasi ya kupata majibu kuhusu masuala mbalimbali waliyouliza kutoka kwa waatalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi waliopo katika maonesho hayo.
Xxxxxxx    xxxxxxx     xxxxxxxx

No comments:

Post a Comment