Kamishna
Msaidizi wa Madini, Uratibu, Mhandisi John Shija akiwaeleza
wanafunzi namna shughuli za uchimbaji madini zinavyofanyika nchini wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la
Wizara ya Nishati na Madini katika Maonesho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
, Jijini Dar es Salaam
Mtaalamu
wa madini ya Vito vya Rangi na Almas Bibi Teddy Goliama kutoka Kitengo cha
Uthamini Madini ya Almas na Vito (TANSORT), Wizara ya Nishati na Madini, akiwaeleza
wanafunzi kuhusu aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini wakati
wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara.
Anayesikiliza wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Uratibu,
Mhandisi John Shija.
Mhandisi Mwandamizi
Masoko na Huduma kwa Wateja, Juliana Pallangyo kutoka Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) akitoa ufafanuzi kuhusu namna Shirika hilo linavyofanya kazi
kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Taasisi hiyo.
1. Afisa
Habari kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Yisambi Shiwa,
akiwaonesha baadhi ya madini yanayopatikana nchini wanafunzi waliotembelea
banda la TMAA.
======== =======
Wanafunzi Dar es Salaam Wavutiwa na Shughuli za
Nishati na Madini
Na
Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Baadhi
ya Wanafunzi kutoka baadhi ya Shule za Sekondari mbalimbali Jijini Dar es
Salaam wametembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini
yake kutaka kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na zinazofanyika.
Wakati
wanafunzi hao walipotembelea Wizara na Taasisi zake, wameoneshwa kuvutiwa na
kutaka kufahamu kuhusu namna shughuli za uchimbaji madini nchini
zinavyofanyika, kutaka kufahamu aina za madini yenye thamani kubwa na madini yenye uzito mkubwa.
Vilevile,
wanafunzi hao wametaka kuelimishwa kuhusu shughuli za utafiti na uchimbaji wa
gesi zinazofanyika nchini ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu vyuo mbalimbali
vinavyotoa mafunzo kuhusu masuala ya gesi, mafuta na madini.
Aidha,
wengi wao walipenda kuona madini ghafi ya Tanzanite yanayopatikana nchini ikiwa
ni pamoja na kufahamu aina zote za madini yaliyopo chini. Wanafunzi hao
wamepata nafasi ya kupata majibu kuhusu masuala mbalimbali waliyouliza kutoka
kwa waatalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi waliopo katika maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment