Meya wa Ilala, Jerry Silaa akifungua rasmi tamasha la kuchangia damu katika
viwanja vya Stakishari, Majumbasita, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo ya siku
10 iliratibiwa na Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa (CCM).
Meya Silaa akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu Salama kabla ya
kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wakiwemo wakina mama wajawazito
katika viwanja vya Sitakishari Majumbasita, Dar es Salaam.
Meya Silaa na Diwani Bonnah wakiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa
maofisa wa damu salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa
wanaoteseka mahospitali kwa kukosa damu.
Meya wa Ilala, Jerry Silaa akiugulia maumivu ya sindano wakati akitoa damu
ili kuwaokoa wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali mbalimbali wakiwemo
wajawazito bila kuwasahau madereva na abiria wa bodaboda wanaoandamwa
na ajali.
Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa naye akidhihirisha azma yake ya kuchangia
damu kwa vitendo katika kilele cha kampeni yake ya kuchangia damu jana
katika viwanja vya Sitakishari, Majumbasita ambapo mamia ya wakazi wa Dar
es Salaam walijitokeza.
Mwakilishi wa Chuo cha Diplomasia, Kennedy Ndosi (katikati)
aliyewahamasisha wanafunzi wa Chuo hicho waliofika kuchangia damu
akiwasikiliza Meya Silaa na Diwani Bonnah wakati wa tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment