Meneja
Masoko wa Mwananchi Communications Ltd (MCL) wachapishaji wa magazeti
ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, Bernard Mukasa akizungumza kwa
njia ya simu katika ofisi za MCL jijini Dar es Salaam jana na mmoja wa
washindi wa bahati nasibu ya Shinda Ki-Brazil ambaye ni fundi umeme,
Issa Rashid Ndingo mkazi wa Kigogo aliyeshinda king’amuzi cha DSTV.
Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na gazeti la Mwanaspoti. Kushoto ni
Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo nchini, Mrisho Millao. Pcha na
Rafael Lubava
Na Mwandishi Wetu
Wasomaji wanne wa gazeti la Mwanaspoti jana Jumatano walitangazwa
kuwa washindi wa kwanza wa promosheni ya Shinda Ki-Brazil na Mwanaspoti
baada ya kunyakuwa zawadi mbalimbali zikiwemo vingamuzi vya Dstv pamoja
na jezi.
Washindi hao wamenyakua zawadi hizo baada ya kutuma neno namba
zitakazopatikana kwenye ukurasa wa tatu wa gazeti la Mwanaspoti kwenda
kwenye namba 15551.Namba moja imetambulishwa kwa herufi B na itamwezesha
mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za binafsi. Namba ya pili
imetambulishwa kwa herufi T na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo
ya zawadi za timu.
Washindi wa vingamuzi vya Dstv pamoja na kifurushi kizima cha malipo
kwa mwezi mmoja (Compact Plus) ni Michael Namenga, Issa Ndingo na
Christopher Chengulla. Kwa upande mwingine aliyejishindia Jozi moja ya
jezi (ina jezi 16), Jackson Fredrick wa Mwanza.
Namenga (54) ambaye ni Afisa Mstaafu wa Jeshi na pia mkazi wa Mbagala
alisema, " Nina furaha sana, nitaendelea kushiriki kwani naamini
nitapata zawadi zingine."
Ndingo (42) ambaye ni mkazi wa Kigogo alisema, " Nawashukuru sana Mwanaspoti, nina uhakika wa kuona Kombe la dunia."
Chengulla (25) ambaye ni mkazi wa Songea mjini, " Jamani someni
Mwanaspoti mfaidi kama mimi, nimebahatika kwasababu nimeshiriki kwa
kipindi kidogo na kushinda."
Fredrick (28) ambaye ni mwalimu alisema, " Nimefurahi kushinda jezi
za kwenye promosheni hii, zawadi hii ni kwa wanafunzi wangu wa timu ya
shule ya Sekondari ya Mamaye iliyopo Misungwi, Mwanza."
Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi, Bernard Mukasa alisema kuwa
bado kuna zawadi nyingi zimebaki kwa wasomaji ambazo ni runinga tatu
zenye ukubwa wa inchi 32, dekoda 27 za Dstv zilizounganishwa na
kifurushi cha compact plus kwa muda wa mwezi mmoja, jozi tano za jezi
pamoja na fedha taslim zinazotolewa kila siku mpaka shindano
litakapomalizika.
Promosheni hii imeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications LTD
(MCL) kupitia gazeti lake la Mwanaspoti kwa kushirikiana na kampuni ya
Multchoice Tanzania (Dstv) ikiwa na lengo la kuwaunganisha wadau wa
soka nchini katika kufurahia mlolongo wote wa matukio ya michuano ya
Kombe la Dunia huko Brazil.
Promosheni hiyo ambayo ilifunguliwa rasmi Juni 2 itafungwa Julai
12 siku ya mwisho ya mashindano hayo ya Kombe la Dunia yatakayofanyika
nchini Brazil.
xxxxxxxx
No comments:
Post a Comment