Msanii Mb Dog pichani.
Mb Dog akamilisha mbili mpya bomba balaa
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI
wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amekamilisha nyimbo
nyingine mbili mpya zinazojulikana kama Ya Moto na Demu Mwingine.
Kukamilika
kwa nyimbo hizo ni mwendelezo wa mikakati ya msanii huyo kufanya kazi
nzuri ili kumuweka katika kiwango cha juu katika tasnia ya muziki wa
kizazi kipya.
Akizungumza
leo mchanaa jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema kwamba nyimbo hizo
amezirekodi katika Studio yake ya Macoppa, zilizopo jijini Dar es
Salaam.
Alisema
kuwa nyimbo hizo zinaungana na ile ‘Mbona Umenuna’ aliyoachia mapema
mwezi uliopita na kupokewa kwa shangwe na wadau wa Bongo Fleva Tanzania.
“Hizi ni nyimbo mbili mpya na ambazo naamini zitapokewa kwa shangwe na wadau mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
“Naamini
kila kitu kitakwenda vizuri kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa mazuri,
ukizingatia kuwa mipango iliyopo mbele yangu ni kufanya kazi ya maana
ili nionyeshe ukomavu wangu kisanaa,” alisema Mb Dog.
Mb
Dog ni mmoja wa wasanii wanaotambulika kwa umahiri wao katika tasnia ya
Bongo Fleva, huku akikumbukwa kwa nyimbo zake, ukiwamo ule wa Latifa na
nyinginezo.
No comments:
Post a Comment