Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unafuraha kuwataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa
kutokana na kukamilika ukarabati wa daraja eneo la bonde la mto Ruvu
mkoani Pwani huduma ya treni ya abiria itaanza upya hapo siku ya Jumanne
Juni 24, 2014 kutoka Stesheni ya Dar es Salaam saa 11 jioni. Wananchi
wanotaka kusafiri wafike stesheni zilizo
karibu yao kwa ajili ya kukata tiketi kuanzia
Juni 19, 2014.
Halikadhalika muda
wa kuondoka treni kwa siku za Jumanne na Ijumaa kutoka Stesheni ya
Dar kwenda Kigoma na Mwanza utakuwa saa 11 jioni na zile za kutoka
Kigoma na Mwanza kuja Dar katika siku za Alhamis na
Jumapili ni saa 11 jioni kutokea Kigoma na saa 12 magharibi kutokea Mwanza.
Jumapili ni saa 11 jioni kutokea Kigoma na saa 12 magharibi kutokea Mwanza.
Tafadhali atakayesoma taarifa hii amuarifu na mwenzake. Uongozi wa TRL unawapongeza wananchi kwa ujumula kwa ushirikiano na uvumilivu waliouonesha wakati wakisubiri kukamilika kwa kazi ukarabati wa njia ya reli.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano ya
TRL kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
TRL kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam,
Juni 18, 2014.
No comments:
Post a Comment