Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto 'kushoto' alivyongoza mashabiki na
wapenzi wa mchezo wa masumbwi kumpokea Ibrahimu Class 'King Class Mawe' aliyeshika mkanda
baada ya kurudi na mkanda wa WPBF kwa kumpiga mzambia Mwansa Kabinga
katika uwanja wa Arthur Davis kwa k,o ya raundi ya tisa na kufanikiwa
kunyakuwa ubingwa uho wa pili kushoto ni bondia Shomari Milundi, kulia
ni Promota aliyefanikisha safari hiyo Yaj Msangi, wadau Bilali Ngonyani
na Rogers Masamu Picha na
www,superdboxingcoach.blogspot.com
www,superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
Bondia Mtanzania anaeshika boxrec
namba moja nchini Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amerudi na ubingwa wa
WPBF nchini akitokeza Zambia ambapo alifanikiwa kumpiga kwa K,O mbaya
sana bondia Mwansa Kabinga wa Zambia mchezo uliochezwa
Arthur Davis Stadium, Kitwe, Zambia
Arthur Davis Stadium, Kitwe, Zambia
akizungumzia
safari yake ya kuelekea kunyakuwa ubingwa huo alisema amepata tabu sana
wakiwa njiani ambapo wame ondoka alhamisi usiku sana na kufika jumamosi
asubui nchini Kenya ambapo alizuiwa kutokana na kuwa na passiport ndogo
hivyo akufanikiwa kwenda Zambia walivyofika kenya waka ongea na Balozi
wa Tanzania wa Kenya akawasaidia ata hivyo ndege waliyokuwa wapande
ilikuwa imesha ondoka zamani
baada ya hapo kuna pesa flani walitakiwa waongeze wakaongeza kiasi kwa kudunduliza wakasafili mpaka Zambia
hata hivyo bondia
huyo ni mchezo wake wa kwanza kucheza nje ya nchi tangia ajiunge na
ngumi za kulipwa na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa huo ambao umemuweka
katika ramani nyingine kabisa ya kimataifa zaidi
pia alishukuru kwa kupokelewa na Mkuu
wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto aliyekuja kwa niaba ya Serekali na
kuahidi kumpatia mmoja ya michezo Kibondo au nchi jirani kwa ajili ya
kumtangaza zaidi na kuendeleza kipaji chake hicho
akitoa ahadi hiyo Mkuu huyo alisema
watu wengi wanapenda mchezo wa ngumi hivyo kwa niaba ya serekali
nitafanya jitiada nikupatie mchezo mmoja kwa ajili ya kutetea mkanda
wako hata burundi ili uzidi kufahamika na kukuza kipaji chako
bondia Ibrahimu Class 'King Class
Mawe' ajawa nyuma kuwashukuru makocha wake ambao wamemwezesha kufika
hapo ambapo ni Habibu Kinyogoli 'Masta' Kondo Nassoro, Sako Mtulya na
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
ambaye anamtafutia mapambano mbalimbali na humpa ushauli awapo ulingoni
No comments:
Post a Comment