Pichani
ni Mtangazaji anayeongoza Kipindi cha 'Mimi na Tanzania' Hoyce Temu
aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 akiwa nje ya Ubalozi
wetu wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kuwasili ambapo alimua
kufunga safari kwa ajili ya kufanya mazungumzo maalum na Balozi wetu wa
Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula.
Mtangazaji
wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akitia saini kitabu cha
wageni kwenye Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani.
Hapa akiwa mapokezi ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani huku akisema ...Naipenda Tanzania yangu!
Hoyce Temu akiangalia baadhi ya picha za Mabalozi 15 ambao tayari
wameshaongoza Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani. wakiwemo Rais
Mstaafu Benjamin William Mkapa, Mustafa Nyang'anyi na Balozi Ombeni
Sefue pamoja Wanawake wawili ambao ni Mama Balozi Mwanaidi Maajar na
Balozi wa sasa Mh. Liberata MulaMula.
Mheshimiwa
Balozi Liberata MulaMula ndani ya mahojiano na mtangazaji wa kipindi
cha Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ofisini kwake jijini Washington DC,
Marekani!
Mahojiano
hayo ya moja kwa moja katika Balozi ya Tanzania nchini Marekani na
Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula ambapo wameangazia masuala
mbalimbali yakiwemo Utalii, kujitangaza katika miradi ya kimaendeleo na
uwekezaji ,malalamiko ya watanzania waishio Marekani kuhusu uraia, kwa
mengineyo mengi usikose kuangalia Channel Ten wiki ijayo Jumapili saa
moja na nusu usiku kilicho bora kabisa.
No comments:
Post a Comment