Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza
Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic
Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi
(NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.
Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa
kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka
Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya
wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo
11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara
mbalimbali.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L.
Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika
mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo
Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali
Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa
mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku
shahada katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi
(NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla
ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika
utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine
vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka nchi
za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia
na Zimbabwe.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao
kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo
Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo
Julai 26, 2014.
Picha ya Pamoja.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment