Mwonekano wa Whisky ya Fyfe,s katika chupa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa, akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho.
Langa Khanyile akitoa ufafanuzi wa Whisky hiyo kabla ya uzinduzi.
Sehemu ulipo fanyika uzinduzi huo katika Hoteli ya Serena.
Wadau mbalimbali wakigongesha glasi zenye Whisky hiyo wakati wa hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakipata kinywaji hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania
Distilleries Ltd (TDL), David Mgwassa (wa pli kushoto), akiwa na baadhi
ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji kipya kiitwacho
Fyfe’s Scotch whisky, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkuu
wa Kitengo cha Masoko wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Kushila Thomas.
Wageni waalikwa wakigongesha glasi lenye kinywaji hicho.
Hapa kinywaji hicho kikipitishwa kwa wageni waalikwa.
Hapa wadau wakinywa na kugongesha glasi za whisky hiyo
Mdau Ngobile Ngwenya akionesha kinywaji hicho.
Hapa wanamuziki wakitoa burudani. |
Wanamuziki hao wakitoa burudani.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa (kulia), akimkabidhi tiketi ya kwenda nchini Scotland, Mshindi wa bahati nasibu ya papo Benard Suma iliyotolewa na TDL. |
Mshereheshaji wa hafla hiyo Jimmy Kabwe
(katikati), akizungumza na mshindi huyo Benard Suma jinsi anavyojisia
baada ya kushinda. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa.
.'
Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd
(TDL) imeendelea kujitanua katika soko nchini baada ya kuzindua kinywaji
kipya cha kimataifa kiitwacho Fyfe's Scotch Whisky.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa
kinywaji hicho Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David
Mgwassa alisema Fyfe's ni kinywaji maridhawa kinachoandaliwa kikamilifu
kikiwa na radha murua na ya kipee.
"Ubora wa kinywaji hiki unatokana na
umahiri mkubwa wa waandaaji na pia unatokana kimea na nafaka bora
zilizotumika na kuwa Fyfe's Whisky huvundikwa kwa miaka kadhaa katika
mji Loch Lomond, Scotland ili kuongeza ubora wake kabla ya kuwa tayari
kwa matumizi" alisema Mgwassa.
Mgwasa aliongeza kuwa kampuni yao
imekuwa ikiwaletea watanzania vinywaji mbalimbali ambavyo vimekuwa
chachu katika kusherehekea hatua tofauti za mafanikio yao na kuendelea
kuwaletea ladha tofauti za vinywaji bora.
Alisema kinywaji hicho ni zawadi ya
pekee katika soko na kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni
kuzinduliwa na baadaye kitazinduliwa nje nyingine.
No comments:
Post a Comment