Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka(kushoto) akikabidhi msaada wa jezi kwa mlinda Mlango wa timu ya soka ya Machava fc |
MAGWIJI wa klabu ya Real Madrid ya Hispania leo
(kesho) wanaendelea na ziara ya
kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika mikoa
ya Arusha na Kilimanjaro ambapo kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa watatembelea lango la kupandia
mlima Kilimanjaro la
Marangu.
Katika ziara hiyo ya kitalii chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)
kimeiteua klabu ya soka inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Panone
FC kuwa wenyeji wa magwiji hao ambao pia watashuhudia mchezo wa
kirafiki kati ya timu za Panone fc na Machava fc utakaopigwa katika
uwanja wa Ushirika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alisema ofisi yake imeandaa
utaratibu wa namna ya kuwapokea magwiji hao pamoja na kuandaa ratiba
maalumu ya kutembelea vivutio ukiwemo mlima Kilimanjaro pamoja
na
kushuhudia mchezo mmoja wa Kirafiki.
“Katika tasnia ya michezo nchi yetu imepata bahati kubwa
ya kutembelewa na wachezaji wa zamani Real Madrid ambao
pamoja na ziara yao wamepanga kutembelea mkoa kwetu ,kikosi hicho
kitaingia kati ya saa tano au saa tano na nusu watashuka uwanja wa
ndege wa KIA,”alisema
Gama.
Alisema baada ya kupokelewa moja kwa moja magwiji hao watapelekwa
Mlima Kilimanjaro katika ofisi za hifadhi ya taifa ya Mlima
Kilimanjaro KINAPA ambako watapata fursa ya kupanda mlima huo kwa
hatua chache baada ya kupokea taarifa ya shughuli za utalii kwa
ujumla.
“Tumewaandalia sehemu ya kupata chakula cha mchana na wenyeji wao
klabu ya Panone fc , baada ya chakula tukasema ni vizuri waone hatupo
mbali katika michezo, kwa hiyo tumepanga kuwa mchezo wa mpira wa miguu
kati ya Panone fc na Machava ikitanguliwa na ikitanguliwa na mechi ya
vijana chini ya miaka 15 .”alisema Gama.
Gama aliwataka wadau na wapenzi wa michezo mkoani humo
kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika mapokezi makubwa ya
wachezaji hao wa zamani na kwamba licha ya kuwa dhamira yao ni
kuimarisha utalii lakini pia wangependa kuona hali ya michezo katika
mkoa wa Kilimanjaro.
“Ni vizuri wakaona hali ya michezo katika mkoa wa Kilimanjaro na
pengine wakapata nafasi ya kuona vipaji vyetu ,mimi ninauhakika hapa
kuna wachezaji wanaweza kuchukuliwa na Real Madrid kwa sababu
tunaweza
kufanya vizuri sana,,,kwa hiyo niwaombe wanamichezo wetu wajitokeze
kwa wingi tukawaone nyota hawa wa Madrid na pengine tuwape ukarimu
wetu wa kitanzania tuliouzoea.”alisema Gama.
Kwa upande wao klabu ya soka ya Panone fc kupitia msemaji wake Kassim
Mwinyi alisema wamefurahishwa na ujio huo na kwamba klabu imejipanga
kujenga mahusiano na magiwji hao kwa lengo la kubadilishana
uzoefu
katika maswala ya michezo.
“Tumepata fursa kama Panone fc ya kukutana na Magwiji hawa wa
Madrid ,sisi tumejipanga kutumia ujio huu katika kujenga mahusiano ya
kitimu kati yetu na wao ,na hakika utakuwa ni mwanzo mwema kwa klabu
yetu
ambayo inajiandaa na ligi daraja la kwanza”alisema Mwinyi.
Magwiji hao watakao ongozwa na wanasoka waliowahi kutamba katika
ulimwengu wa soka kwenye ligi kuu ya Hispania maarufu kama La
Liga,ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Bacrays,michuano ya Mabingwa
na ile ya kombe la dunia wakiwa na nchi zao wameanza kuwasili nchini
kwa ajili ya ziara maalumu.
Baadhi ya Wanandinga hao wa zamani waliotamba na Real Madrid kwenye
michuano ya La Liga, UEFA pamoja na kombe la dunia wakiwa na nchi zao
watakaofanya ziara ya siku nne nchini ni pamoja na Zinedine zidane,
Luis Figo, Fabio Cannavaro, Ronaldo De Lima, Christian karembeu
na
Michael Owen.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya kaskazini,
No comments:
Post a Comment