Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono na Mkurugenzi
wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela wakati wa kubadilishana mikataba
baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya Radio
hiyo,yaliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji
mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge
amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini
Dar Es salaam leo.
Kutokana
na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa
zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini
Tanzania.
Mkurugenzi
wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwake kwa
mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.
“Mpaka
sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia
kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema
mkuregenzi huyo.
Maulidi
Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji walio bobea
katika fani hiyo akiwemo Dizo one,Dennis Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na
Dj Majay.
No comments:
Post a Comment