Emmanuel Okwi karudi nyumbani Msimbazi |
Okwi aliyekuwa akiichezea Yanga imedaiwa amekamilisha usajili wake wa kukipiga Simba na tayari jina lake ni miongoni mwa majina 29 yaliyopelekwa TFF kwa ajili ya kuombewa usajili kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza Septemba 20.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba, Zakaria Hanspope amethibitisha kumsainisha miaka miwili mshambuliaji huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Uganda The Cranes.
Kurejea kwa Okwi ndani ya Msimbazi ni kama imeirahisishia kazi Yanga iliyokuwa njia panda kuamua nani ikate jina lake kati ya nyota wake wa kigeni sita waliokuwa wapo kwenyue kikosi chao.
"Ni kweli Okwi tumemsajili kwa miaka miwili na atakuwa kwenye kikosi cha Simba kwa msimu ujao," Hanspope amenukulia akisema kwa kujiamini.
Yanga ilikuwa katika sintofahamu ya kuamua imuache nani kati ya Okwi na Jaja Brazil aliyepigiwa debe na kocha Marcio Maximo, ambaye hata hivyo uongozi ya Jangwani ulikuwa haujaridhika naye.
Hayo yakijiri TFF imeongeza siku mbili zaidi za usajili wa wachezaji wa ndani ingawa zoezi hilo lililikuwa limekamilika usiku wa jana.
Kwa usajili wa Mapro zoezi litaendelea hadi Jumamosi ijayo yaani Septemba 6.
No comments:
Post a Comment