Mwanasheria mkuu wa CHADEMA akizungumza na wanahabari muda huu |
Chama
cha democrasia na maendeleo CHADEMA leo kimetangaza kuwa mwenyekiti wao
keshoi ataenda polisi makao makuu kuitikia wito wa jeshi hilo ambao
ulikuja kwa barua ukimhitaji mwenyekiti huyo kufika makao makuu ya jeshi
hilo.
Kauli
hiyo imetangazwa muda huu makao makuu ya chama hicho na wanasheria mkuu
wa chama hicho mbunge TUNDU LISSU wakati akizungumzia wito wa jeshi la
polisi kumhitaji mwenyekiti wao kwa kile ambacho ameadi kuwa hakijawekwa
wazi wanamwitia nini.
"Tumepokea
barua ya jeshi la polisi makao makuu wakimtaka mwenyekiti wetu kufika
makao makuu ya polisi kwa maelezo,kamati kuu ya chama imeridhia
mwenyekiti aende ila hawezi kwenda mwenyewe hivyo wanasheria wote wa
chama walioko mkoani Dar es salaam watamsindikiza kwa ajili ya kujua
mwenyekiti wetu ameitiwa nini.hivyo tunaomba wanasheria wote wa chama
kesho tukutane polisi makao makuu saa tano kwa ajili ya kumsindikiza.
Naibu katibu mkuu wa chama JOHN MNYIKA akizungumza |
Aidha
naibu katibu mkuu wa chama hicho mh JOHN MNYIKA NAYE naye amewataka
wananchi na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kesho kumsindikiza
mwenyekiti wao kwa ajili ya kusikiliza kile ambacho mwenyekiti wao
ameitiwa nini na jeshi la polisi.CREDIT DJ SEK BLOG
No comments:
Post a Comment