Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Biashara kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Bw. Abdulla Makame Akiwaeleza waandishi wa Habari(hawapo
pichani) Kuhusu Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu
Jijini Arusha. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara
hiyo Anthony Ishengoma.
Picha na Hassan Silayo
Frank Mvungi- Maelezo
Mkutano
wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati za kusafiria za
kielektroniki, zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi, za
Maofisa na za kawaida.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Biashara,Uwekezaji na shughuli za uzalishaji wa Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Dk. Abdulla Makame wakati wa mkutano na waandishi wa
habari.
Mkutano
huo utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha pia unatarajia
kupokea na kuidhinisha taarifa mbalimbali sambamba na kutolea maamuzi
masuala yanayohusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akieleza
zaidi Makame amesema mkutano huo utapokea na kuidhinisha aina mpya ya
hati ya kusafiria ya kielektroniki,zikiwemo sampuli za hati za kusafiria
za kibalozi, za Maofisa na za kawaida za kusafiria.
Aidha
Mkutano huo utajadili mapendekezo na hadidu za rejea za uanzishwaji wa
Dira ya maendeleo ya Afrika Mashariki ya mwaka 2050.
Pia
mkutano huo utajadili mapendekezo ya mpango mwelekeo na shughuli
mbalimbali zinazolenga kuandaa katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki
na kujadili mapendekezo ya baraza la ulinzi na usalama linalopendekezwa.
Baraza
la Mawaziri katika Jumuiya ya Afrika mashariki ni chombo cha pili
katika ngazi za kufanya maamuzi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
baada ya Mkutano wa Kilele.
No comments:
Post a Comment