Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
(kulia) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa
mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam. Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti 'IP Pop'
Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter
Ngota (kushoto) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau
wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL.
Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter
Ngota (kushoto) akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti 'IP Pop'
Ofisa Mratibu wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Anifa Chingumbe (kushoto) akimwelezea. Baadhi ya wadau washiriki katika mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL wakifuatilia mkutano huo.
KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) imeanzisha
kituo cha kuuzia huduma za interneti 'IP Pop -Internet Protocol Point of
Presence' nchini ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma za mawasiliano
zaidi. Huduma kama hii awali ilikuwa ikinunuliwa nje hasa makampuni
anuai yanayotoa huduma hizo barani ulaya.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu Mauzo na
Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota alipokuwa
akizungumza na wanahabari katika mkutano wa wadau anuai wa mawasiliano
kutoka nchi za Afrika Mashariki na baadhi za mataifa ya Afrika
unaofanyika Tanzania. Ngota alisema kampuni ya TTCL imekuwa na mchango
mkubwa wa kusimamia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwawezesha
Watanzania na hata nchi jirani kupata mawasiliano mazuri kutoka katika
nchi zao hadi katika nchi za ulaya.
"...Kuna juhudi mbalimbali TTCL tunafanya ili kuongeza fursa kwenye
mawasiliano ambapo kwa sasa tumefungua kituo cha kuuzia interneti hapa
nchini, kinaitwa IP Pop (Internet Protocol Point of Presence). Awali
interneti tulikuwa tunaenda kununulia London kwenye makampuni mbalimbali
sasa hivi tumeanzisha kituo chetu cha kununulia intaneti hapa hapa
nchini...Kwa hiyo tunawakaribisha watumiaji wa interneti kuja kununua
huduma hizi kwetu," alisema Ngota.
Akizungumzia mkutano huo, Ngota alisema wadau wa mawasiliano Afrika
ikiwemo TTCL imejipanga vizuri kutumia fursa ambazo zinaweza kupatikana
nchini na nje ya nchi ili kuendeleza sekta ya mawasiliano. "...Unapopiga
simu lazima uende hadi nchi za nje kupata ile njia alafu ndo unarudi
ulipo Afrika sasa hivi tunaangalia namna gani tutajikwamua na huduma
kama hizo kuzipata hapa hapa Afrika..." alisema ofisa huyo wa TTCL.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
January Makamba akizungumzia mkutano huo alisema mkutano huo ni muhimu
kwani wadau wa mawasiliano wamekutana kujadili maendeleo ya sekta ya
mawasiliano, hasa katika ukanda wa afrika mashariki na afrika kwa
ujumla. Alisema Tanzania inategemewa sana na nchi karibia saba ambazo
zipo pembezoni mwa bahari kupitia huduma ya mkongo wake wa mawasiliano.
"Mkongo wa mawasiliano wa kimataifa umetua katika bahari yetu na sisi
tunauza huduma hiyo kwa nchi nyingine...Tumeupeleka hadi kwenye mipaka
ya majirani zetu kama Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na wengineo ambao
hawana mawasiliano."
Makamba alisema mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata
mawasiliano mazuri na yalio bora maana hiyo ni haki yake. Sera na
kanuni za Serikali ni kuhakikisha hilo linafanikiwa. Aliongeza kuwa kwa
kulitambua hilo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kujenga
mkongo wa taifa wa mawasiliano.
"..Na sasa tunaingia kwenye awamu ya tatu ya upanuzi wa mkongo huo ikiwa
ni sambamba na uboreshaji wa mawasiliano, ili ufike kila wilaya nchini,
Watanzania wengi maeneo ya vijijini bado hawana mawasiliano, sehemu
nyingine hakuna mawasiliano kabisa au pengine yapo lakini si mazuri.
Aidha alibainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka
2015 maeneo yote ambayo hayana mawasiliano yanapata mawasiliano, hii ni
pamoja na kukaribisha makampuni mapya yaweze kuwekeza katika sekta hii
ili uwepo ushindani kwamba kama kuna maeneo kampuni fulani haitaki
kwenda basi nyingine ziende huko.
"...Mkongo wa taifa wa mawasiliano ni biashara na majirani zetu
wanategemea na wananunua huduma hiyo kutoka kwetu. Tunachokifanya ni
kuiimarisha kampuni ya TTCL hadi sasa wanafanya kazi nzuri sana wana
wadau na washirika wengi toka nchi jirani ambapo wanafanya nao biashara.
Kazi ya Serikali ni kuiwezesha ili biashara hiyo iwe kubwa zaidi,"
alisema Makamba.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment