Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza
wakati alipokuwa akilihutubiua Taifa katiuka mkutano wake na Wazee
uliofanyika jioni hii kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam. Katika Hotuba yake Mhe. Rais alizungumzia suala la sakata la
fedha za Escrow na kutaja mapendekezo na maamuzi ya Kamati maalum ya
Bunge la Jamhuri kuhusu suala hilo na kutangaza rasmi kumfuta kazi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka,
kutokana na kuhusishwa moja kwa moja na upokeaji wa fedha hizo.
Mapema
wiki iliyopita. Prof. Tibaijuka aliitishja mkutano na wanahabari na
kutangaza rasmi dhamira yake ya kutojiuzulu katika wadhfa wake huo kwa
kile alichodai kutohusika na moja kwa moja na suala hilo, huku
akijitetea kuwa fedha hizo zilitumwa kwake kwa ajili ya msaada wa shule.
Baada
ya Mhe. Rais kutangaza maamuzi hayo ya kumfuta kazi Prof Tibaijuka,
ukumbi huo uliripuka kwa shangwe na vigeregere vya kumpongea Rais kwa
maamuzi hayo, huku kwa upande wa Prof. Mhongo, ikielezwa kuwa suala lake
bado linafanyiwa kazi na uchunguzi utakapokamilika basi nalo litatolewa
maamuzi.
Rais
Jakaya Kikwete, akiendelea kuzungumza na Wazee, ukumbini hapo (kushoto)
ni Makamu wa Rais, Dkt. Mhammed Gharib Bilal, na (katikati) ni Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza, kumsikiliza mhe. Rais.
Baadhi ya mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi, waliohudhuria.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, akitafakari hotiba ya Rais Jakaya.
Viongozi wa dini waliohudhuria
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, wakati akiondoka ukumbini hapo.
No comments:
Post a Comment