Mhe
Ummy Mwalimu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais akifungua mafunzo kwa wasichana wa Wilaya ya Muheza juu ya
kujitambua na kujithamini katika masuala ya Afya ya uzazi. Mafunzo hayo
yamefanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Muheza.
Mhe.
Ummy Mwalimu, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais kupitia Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake wa Mkoa wa Tanga
(TAWODE) ameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana wa Wilaya ya Muheza,
Mkoani Tanga wenye umri kati ya miaka 10 - 24. Lengo la mafunzo hayo ni
kuwawezesha wasichana hao kujitambua na kujithamini katika masuala ya afya ya uzazi ili kujikinga na mimba na ndoa za
utotoni na maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Mhe Ummy Mwalimu Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais akiwa katika picha
ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kujitambua na kujithamini Wilayani Muheza
mwishoni mwa wiki.
Wasichana wa Wilaya ya Muheza wakifanya
majadiliano na mawasilisho katika vikundi juu ya changamoto wanazokumbana nazo
katika kipindi cha ujana.
Wasichana wa Wilaya ya Muheza wakifanya
majadiliano na mawasilisho katika vikundi juu ya changamoto wanazokumbana nazo
katika kipindi cha ujana.
No comments:
Post a Comment