Kamati
ya Miss Universe Tanzania imemteua mshindi wa pili wa Miss Universe 2014, Nale
Boniface kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe yatakayofanyika mwanzoni mwa
mwezi wa kwa kwanza 2015 Miami, Marekani.
Hatua
hii imechukuliwa baada ya mshindi husika Miss Universe Tanzania 2014, Carolyne Bernard kupata ajali na kuvunjika
kidole chake cha mguu. Ripoti ya daktari imeonyesha kuwa kupona kwake
kutachukua mwezi mmoja wakati mrembo anatakiwa awe mashindanoni baada ya siku
kumi kuanzia sasa. Isitoshe awapo mashindanoni mrembo atapaswa kuvaa viatu
virefu (High heels) wakati wote ambapo haishauriwi kiafya kutokana na tatizo
lake.
Hivyo
kutokana na hali hii, Nale Boniface ambaye alishika nafasi ya pili na
aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth ndiye atakayekwenda
kuiwakilisha nchi badala yake kama mkataba unavyoainisha na hivyo atakuwa Miss
Universe Tanzania 2014.
Kamati
inasikitishwa na kuumia kwa Carolyne na inaahidi kuendelea kuwa nae bega kwa
bega katika matibabu yake kwani bado yupo chini ya mkataba wa Miss Universe
Tanzania kwa mwaka mzima.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania mwaka huu yalifanyika tarehe 31 mwezi wa Kumi na
yalidhaminiwa na Insignia, Golden Tulip,
Compass Communications, AzH Photography,
No comments:
Post a Comment