Sunday, January 18, 2015

Waziri Mahanga azindua kitabu cha Marehemu Steven Kanumba


NAIBU Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga,  jana amezindua rasmi kitabu cha marehemu Steven Charles Kanumba, Kinachoitwa ''Steven Charles Kanumba: The Great Fallen Tree''  kilichoandikwa na Emmanuel Zirimwabagabo, raia wa Congo anayeishi nchini Canada.
Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu kama marehemu Kanumba na si kulalamika kila siku,  jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.
Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha Kanumba, ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kukisambaza dunia nzima.
Alisisitiza kwamba vizazi vijavyo ambavyo havikumuona vitamfahamu muigizaji huyo nguli wa Tanzania kupitia kitabu hicho kilichozungumzia maisha yake yote ya enzi za uhai.
Wasanii mbalimbali wa filamu walihudhuria uzinduzi huo huku bendi ya Malaika chini ya Christian Bella ilitumbuiza kusindikiza uzinduzi huo.
(Na Gabriel Ng'osha/GPL).
KINANA AAHIDI USHINDI WA KISHINDO KWA CCM ZANZIBAR 2015 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyeka majani mbele ya Chuo cha Sayansi ya Bahari (IMS), alipotembelea chuo hicho kilicho chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Buyu, Unguja Zanzibar leo wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG Kinana akikagua jengo jipya la Chuo cha Sayansi ya Bahari. Ameahidi mbele ya uongozi wa chuo hicho kuwa ataibana Serikali itoe fedha ilizoahidi kumalizia ujenzi wa chuo hicho ambacho ujenzi wake ulianza mwaka 2004 lakini hadi sasa haujakamilika. Kinana akiangalia samaki aina ya kaa akijiandaa kupanda karibu na ufukweni wakati wa ziara yake katika Jimbo la Fueni, Unguja, Zanzibar leo. Kinana akipanda samaki aina ya kaa katika ufukwe wa Bahari eneo la Fuoni Zanzibar Kinana akikagua shamba la mikoko baada ya kushiriki kuipanda. Aliwasifu wananchi wa Jimbo la Fuoni kwa kuhifadhi mazingira. Kinana akipita kwenye mikoko Kinana akikata ki kwa kunywa maji ya dafu baada ya kushiriki kupanda samaki aina na kaa na mikoko Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hdhara kwenye Uwanja wa Magereza Kijiji cha Tomondo, Dimani Mkoa wa Magharibi, Zanzibar. Amewahakikishia wana CCM kwamba wajiandae kushinda kwa kishindo katika uchaguzi Mkuu ujao mwaka huu na kuwataka wajenge mshikamano. Pia Kinana aliwataka viongozi kuchagua wagombea wanaopendwa na wananchi si wanaolazimisha kushinga uongozi kwa kutumia fedha. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Magereza, Katika Kijiji cha Tomondo, Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Magharibi, ambapo alimtaka Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), ajiuzulu kutoka kwenye Serikali ya Shirikisho baada ya kutofautiana na kuhusu muundo wa muungano ambapo yeye anataka Serikali tatu na wa mkataba, wakati serikjali iliyopo inataka muundo wa sreikali mbili. Kinana akisalimiana na wanachama wa CCM alipowasili katika mkutano wa halmashauri ya Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Magharibi, Zanzibar. Kulia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Idd Seif Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma wakati Kinana alipowasili kwenye mkutano huo Akia mama wakimshamngilia wakati wa mapokezi ya Kinana katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Dimani Kinana akikagua kiwanda cha maziwa cha Azam Diary Products Ltd, kilichopo Fumba, Unguja, Zanzibar Kinana akiangalia maziwa yanayozalishwa katika kiwanda hicho. Kulia ni Meneja wa kiowanda hicho Kartikumar Dave Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akipakia makasha ya maziwa kwa Folk Lift wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokwenda kukagua Kiwanda cha maziwa cha Azam kilichopo Fumba, Unguja Zanzibar Kinana akizawadia kasha la maziwa Kinana akikata utepe kuzindua rasmi gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Fuoni, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa katika jimbo hilo.. Wananchi wakishangilia wakati Kinana akihutubia katika mkutano wa hdhara kwenye Uwanja wa Magereza, Kijiji cha Tomondo, Ali Aman Abeid Karume akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo aliwashauri wazanzibar kumomba Ali Mohamed Shein kugombea tena urais wa Zanzibar kwa vile katika kipindi cha uongozi wake amefanya makubwa. Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Ali Vuai Nahodha akihutubia katika mkutano huo wa hadhara.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

No comments:

Post a Comment