NAIBU Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga, jana
amezindua rasmi kitabu cha marehemu Steven Charles Kanumba, Kinachoitwa
''Steven Charles Kanumba: The Great Fallen Tree'' kilichoandikwa na
Emmanuel Zirimwabagabo, raia wa Congo anayeishi nchini Canada.
Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu kama marehemu Kanumba na si kulalamika kila siku, jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.
Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha Kanumba, ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kukisambaza dunia nzima.
Alisisitiza kwamba vizazi vijavyo ambavyo havikumuona vitamfahamu muigizaji huyo nguli wa Tanzania kupitia kitabu hicho kilichozungumzia maisha yake yote ya enzi za uhai.
Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu kama marehemu Kanumba na si kulalamika kila siku, jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.
Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha Kanumba, ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kukisambaza dunia nzima.
Alisisitiza kwamba vizazi vijavyo ambavyo havikumuona vitamfahamu muigizaji huyo nguli wa Tanzania kupitia kitabu hicho kilichozungumzia maisha yake yote ya enzi za uhai.
Wasanii mbalimbali wa filamu walihudhuria uzinduzi huo huku bendi ya
Malaika chini ya Christian Bella ilitumbuiza kusindikiza uzinduzi huo.
(Na Gabriel Ng'osha/GPL).
(Na Gabriel Ng'osha/GPL).
KINANA AAHIDI USHINDI
WA KISHINDO KWA CCM ZANZIBAR 2015
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyeka majani mbele
ya Chuo cha Sayansi ya Bahari (IMS), alipotembelea chuo hicho kilicho
chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Buyu, Unguja Zanzibar leo
wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi
inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza
kero za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kinana akikagua jengo jipya la Chuo cha Sayansi ya Bahari. Ameahidi
mbele ya uongozi wa chuo hicho kuwa ataibana Serikali itoe fedha
ilizoahidi kumalizia ujenzi wa chuo hicho ambacho ujenzi wake ulianza
mwaka 2004 lakini hadi sasa haujakamilika.
Kinana akiangalia samaki aina ya kaa akijiandaa kupanda karibu na
ufukweni wakati wa ziara yake katika Jimbo la Fueni, Unguja, Zanzibar
leo.
Kinana akipanda samaki aina ya kaa katika ufukwe wa Bahari eneo la
Fuoni Zanzibar
Kinana akikagua shamba la mikoko baada ya kushiriki kuipanda. Aliwasifu
wananchi wa Jimbo la Fuoni kwa kuhifadhi mazingira.
Kinana akipita kwenye mikoko
Kinana akikata ki kwa kunywa maji ya dafu baada ya kushiriki kupanda
samaki aina na kaa na mikoko
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa
hdhara kwenye Uwanja wa Magereza Kijiji cha Tomondo, Dimani Mkoa wa
Magharibi, Zanzibar. Amewahakikishia wana CCM kwamba wajiandae kushinda
kwa kishindo katika uchaguzi Mkuu ujao mwaka huu na kuwataka wajenge
mshikamano. Pia Kinana aliwataka viongozi kuchagua wagombea wanaopendwa
na wananchi si wanaolazimisha kushinga uongozi kwa kutumia fedha.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika
mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Magereza, Katika Kijiji cha Tomondo,
Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Magharibi, ambapo alimtaka Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi
(CUF), ajiuzulu kutoka kwenye Serikali ya Shirikisho baada ya
kutofautiana na kuhusu muundo wa muungano ambapo yeye anataka Serikali
tatu na wa mkataba, wakati serikjali iliyopo inataka muundo wa sreikali
mbili.
Kinana akisalimiana na wanachama wa CCM alipowasili katika mkutano wa
halmashauri ya Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Magharibi, Zanzibar. Kulia ni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Idd Seif
Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma wakati Kinana alipowasili kwenye mkutano
huo
Akia mama wakimshamngilia wakati wa mapokezi ya Kinana katika Ofisi ya
CCM Wilaya ya Dimani
Kinana akikagua kiwanda cha maziwa cha Azam Diary Products Ltd,
kilichopo Fumba, Unguja, Zanzibar
Kinana akiangalia maziwa yanayozalishwa katika kiwanda hicho. Kulia ni
Meneja wa kiowanda hicho Kartikumar Dave
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akipakia makasha ya
maziwa kwa Folk Lift wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
alipokwenda kukagua Kiwanda cha maziwa cha Azam kilichopo Fumba, Unguja
Zanzibar
Kinana akizawadia kasha la maziwa
Kinana akikata utepe kuzindua rasmi gari la kubebea wagonjwa
lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Fuoni, kwa ajili ya kuhudumia
wagonjwa katika jimbo hilo..
Wananchi wakishangilia wakati Kinana akihutubia katika mkutano wa
hdhara kwenye Uwanja wa Magereza, Kijiji cha Tomondo,
Ali Aman Abeid Karume akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo
aliwashauri wazanzibar kumomba Ali Mohamed Shein kugombea tena urais wa
Zanzibar kwa vile katika kipindi cha uongozi wake amefanya makubwa.
Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Ali Vuai Nahodha akihutubia katika
mkutano huo wa hadhara.
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
No comments:
Post a Comment