Na
Greyson Mwase, Maswa.
Meneja Utaalamu Elekezi kutoka
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Gissima Nyamohanga amesema kuwa serikali imetumia shilingi bilioni 881 katika
mradi wa kusambaza umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya
Pili.
Nyamohanga aliyasema hayo
kwenye sherehe za uzinduzi wa mradi wa
umeme vijijini unaofadhiliwa na REA uliofanyika katika kata ya Shishiyu
wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Alisema kuwa Mradi wa REA
Awamu ya Pili utaiwezesha idadi ya
vijiji vilivyounganishwa na umeme 3734 kati ya vijiji 15,180 ambayo ni asilimia 24.6
kufikia vijiji 5,234 ambayo ni asilimia 34.5 ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Aliongeza kuwa mradi wa REA
Awamu ya Pili wa miaka miwili ulioanza
mwaka 2013, lengo lake lilikuwa ni
kuhakikisha kuwa vijiji vyote Tanzania vinapatiwa umeme hivyo kuboresha
maisha ya wananchi na kukuza uchumi wa
nchi.
Akielezea mchango wa mradi wa
usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na REA katika kuboresha maisha ya wananchi Nyamohanga alisema kuwa awali
wananchi wote walikuwa wakilipa shilingi
467,000 kama gharama ya
kuunganishiwa umeme ambayo ilikuwa ni kubwa na kupelekea wananchi wachache wenye uwezo kuwa na nishati ya
umeme huku ikiacha kundi kubwa la
wasio na uwezo kuishi gizani.
Alisema kuwa katika Awamu ya
Kwanza ya REA gharama za uunganishaji wa umeme
zilishuka kutoka shilingi 467,000
hadi shilingi 177,000 na kuongeza kuwa katika kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uwezo wa
kuunganishiwa umeme Serikali
iliamua kubeba gharama zote kupitia REA Awamu ya Pili na
wananchi kutakiwa kuchangia shilingi 27,000 tu kama kodi ya ongezeko (VAT)
Alieleza kuwa mara baada ya
kumalizika kwa Awamu ya Pili ya REA,
viongozi wataainisha vijiji ambavyo
havijapata umeme REA Awamu ya Pili,
ambapo vitajumuishwa katika mradi wa REA Awamu ya Tatu.
Nyamohanga alieleza michango
mingine kuwa ni kufungua fursa za ajira na uwekezaji kwa vijana wa
kitanzania, ufaulu kuongozeka kwa shule
za sekondari na kuboreshwa kwa huduma za afya.
“Kwa mfano kwa shughuli za
kiuchumi bei ya kusaga debe la mahindi
ilikuwa ni shilingi 1,000 itashuka hadi
shilingi 500 kutokana na kwamba mashine
za kusaga zitakuwa zinatumia umeme badala
ya dizeli kama zamani,” alisema
Nyamohanga
Wakati
huohuo
Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda
ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma akielezea jinsi ya
kuunganishwa na huduma ya umeme kwa wananchi wa vijiji vilivyopitiwa na mradi wa REA Awamu ya Pili alisema kuwa wananchi
wanaoishi mita 30 karibu na miundombinu
ya umeme wataunganishiwa kwa shilingi
27,000 na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kuboresha makazi yao.
Alisema
kwa wananchi wenye nyumba zenye vyumba viwili na vioski hawahitaji kufunga
mfumo wa umeme kwenye nyumba zao (wiring) badala yake watashauriwa kununua
kifaa maalumu kijulikanacho kama “UMETA” (Umeme Tayari) kinachoweza kutumika
kama mfumo kwa kuwa na uwezo wa kuunganisha taa mbili na vifaa vingine kama
vile jiko, friji na pasi.
Aliendelea
kusema kuwa kifaa hicho kinachouzwa kwa gharama ya shilingi 37,000 kitakuwa ni
mali ya mteja na endapo atahama makazi basi atakuwa huru kuhama pamoja na kifaa
chake.
Airtel kuzindua Airtel
UNI 255 J-mosi maalum kwa Wanafunzi UDSM katika Viwanja vya Mabibo
Hostel Afisa Masoko wa Airtel Henrick Bruno akionyesha moja kati ya
vocha za Airtel UNI255 maalum kwa vyuo vikuu nchini tayari kwa uzinduzi
jumamosi hii. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX · Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki,
Shilole kupamba uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UDSM Kampuni ya simu
za mkononi ya Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii
itazindua rasmi huduma mpya maalum kwaajili ya kutoa huduma nafuu za
mawasiliano kwa wanafunzi walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es
salaam UDSM ambapo hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama
Airtel UNI 255 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika
viwanja vya Mabibo hostel Akiongea kuhusiana na uzinduzi wa huduma hiyo
Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni
huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye
kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo
wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma
hiii ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti,
kupiga simu na hata sms. Huduma hii tayari tumeshaizindua kwa vyuo vikuu
vingine vya Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza na imeonyesha mafanikio
makubwa sana kwa watumiaji wakiwemo wanafunzi na wale wote wanaotumia
huduma hii maeneo ya vyuo” “Airtel tumeona ni vyema tuizindua hapa
katika vyuo vya Dar es salaam wiki hii siku ya Jumamosi pale mabibo
hostel ambapo mbali na uzinduzi kutakuwa na tamasha kubwa litakalopambwa
na watoa burudani nguli akiwemo Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole
pmaoja na DJ maarufu jiji Dj Zero aliongeza kusema Mmbando Nae meneja wa
huduma hiyo ya UNI 255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana hii ni
huduma maalum kwa wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema kuizindulia
katika Hostel zao pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi wengi wa chuo
kikuu hapa jijini wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo wanakaribishwa
katika uzinduzi huo ambapo kiingilo chake ni BURE” Burudani zitakuwa
zakutosha kupitia Airtel UNI 255 siku hiyo. Kampuni ya simu za mkononi
ya airtel ilianzisha huduma ya UNI255 ili kuendana sambamba na mkakati
wao wa kusaidia vyuo vikuu nchini kutumia ipasavyo huduma za mtandao ili
kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la kusaidia wateja wake walioko
vyuoni kufikia malengo yao.
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
No comments:
Post a Comment