BENDI MPYA
•Vijana Ngwasuma ilizinduliwa ndani ya Letasi Lounge
(zamani Business Park ,Victoria) Ijumaa ya tarehe 07-Mar-2014.
•Yamoto Band yazinduliwa rasmi tarehe 21-Sep-2014 ndani
ya ukumbi wa Dar Live Mbagala.
•Utalii Band yazinduliwa Ijumaa ya
tarehe 26-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa MRC (Mikocheni Resort Centre)
•Kundi la Chuchu Sound liliibuka tena na kupiga show
kadhaa katika ukumbi wa Max Bar Ilala. Baadaye kwa sababu kadhaa bendi ikapotea.
•Pia kulikuwa na bendi ambazo sio mpya lakini ndani ya
mwaka 2014 ziliundwa upya. Bendi hizi ni Victoria Sound na Ruvu Stars.
•Bendi nyingine zilizoanzishwa ndani ya mwaka 2014 ni JJ
Band, bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika
hotel ya Jembe ni Jembe. Pia kuna Ruby Band. Bendi hizi 2 zinatarajiwa
kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2015.
UZINDUZI WA ALBUM MPYA
•Extra Bongo walizindua album ya “Mtenda Akitendewa”
Jumamosi ya tarehe 22-Feb-2014 ndani ya Dar Live Mbagala.
•Talent Band (ya Hussein Jumbe) wazindua album ya “Kiapo
Mara Tatu” Jumatano ya 30-Apr-2014 ndani ya Kisuma Night Pub, Temeke (zamani
Sugar Ray)
•Christrian Bella azindua album ya “Nani Kama Mama” ndani
ya Mzalendo Pub Jumamosi ya tarehe 30-Aug-2014
•Tarsis Masela katika viunga vya Ten Lounge (Business
Park) Victoria azindua album ya “Acha Hizo” Ijumaa ya tarehe 21-Nov-2014
•Mashujaa Band yazindua album ya “Ushamba Mzigo” kwenye
ziara za mikoani.
KILI MUSIC AWARD
•Kili Music Award 2014 ilifanyika Jumamosi ya tarehe
03-May-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele
(categories) 8 vya muziki wa dansi.
Washindi walikuwa kama ifuatavyo;
1. Mwimbaji Bora wa Kiume-Jose Mara (Mapacha Watatu)
2. Mwimbaji Bora wa Kike-Luiza Mbutu (Twanga Pepeta)
3. Rapa Bora-Fergusson (Mashujaa Band)
4. Wimbo Bora-Ushamba Mzigo (Mashujaa Band) 5. Bendi Bora-Mashujaa Band 6. Mtunzi Bora-Christian Bella (Malaika Music Band) 7. Producer Bora-Amorosso 8. Hall of Fame (Individual)-Hassan Rehani Bitchuka (Mlimani Park Orchestra)
1. Mwimbaji Bora wa Kiume-Jose Mara (Mapacha Watatu)
2. Mwimbaji Bora wa Kike-Luiza Mbutu (Twanga Pepeta)
3. Rapa Bora-Fergusson (Mashujaa Band)
4. Wimbo Bora-Ushamba Mzigo (Mashujaa Band) 5. Bendi Bora-Mashujaa Band 6. Mtunzi Bora-Christian Bella (Malaika Music Band) 7. Producer Bora-Amorosso 8. Hall of Fame (Individual)-Hassan Rehani Bitchuka (Mlimani Park Orchestra)
WANAMUZIKI WALIOFARIKI
•Mpiga tumba wa Twanga Pepeta Soud Mohamed “MCD” afariki
dunia Jumatatu ya tarehe 27-Jan-2014
•Mpiga bass wa Vijana Jazz, Maulid Mwangia afariki
Jumatano tarehe 12-Mar-2014 na kuzikwa Alhamis tarehe 13-Mar-2014
•Mwanamuziki mkongwe Muhiddin Gurumo afariki dunia Jumapili
ya tarehe 13-Apr-2014 na kuzikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe Jumanne ya
tarehe 15-Apr-2014
•Mpiga gitaa wa Skylight Band, Chili
Challa wa Skylight Band afariki dunia tarehe 17-Apr-2014.
•Amina Ngaluma “Japanese” afariki tarehe 15-May-2014 akiwa mji wa Phuket, Thailand.
•Mwanamuziki DIGITAL wa FM Academia afariki Ijumaa tarehe
18-Jul-2014.
•Ally Rashid “Mwana Zanzibar” ambaye mara ya mwisho
alikuwa mpuliza sax wa Msondo Ngoma afariki tarehe 10-Oct-2014.
•Suzuki Sauti ya Malaika aliyepigia Extra Bongo katika
album ya “Mjini Mipango” alifariki tarehe 15-Oct-2014
•Mwanamuziki Khamis Kayumba “Amigoulaus” afariki tarehe
09-Nov-2014.
•Mwanamuziki Shem Ibrahim Kalenga afariki dunia
15-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 16-Dec-2014 katika makaburi ya Kisutu.
•Mnenguaji Aisha Madinda afariki dunia tarehe 17-Dec-2014
na kuzikwa tarehe 19-Dec-2014.
MATUKIO MENGINE MAKUBWA
•Mdahalo wa kwanza wa aina yake wa kujadili muziki wa
dansi wafanyika katika ofisi za TBC Jumamosi ya tarehe 05-Apr-2014 chini ya
u-moderator wa Dacota Khamis, kuhudhuriwa na wadau karibia 30 na kuonyeshwa
live na TBC2 na baadaye kuonyeshwa recorded na TBC1 kwenye kipindi cha
“Nyumbani ni Nyumbani”
•Bendi ya Msondo Ngoma yafanya sherehe za maadhimisho ya
kutimiza miaka 50. Maadhimisho yalianza Ijumaa ya tarehe 10-Oct-2014 ndani ya
Leaders Club na kuhitimishwa TCC Chang’ombe Jumamosi ya tarehe 01-Nov-2014. Pia
wanamuziki wa bendi walikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais
Jakaya Kikwete, Alhamis ya tarehe 30-Oct-2014.
•Kwa mara ya kwanza tukio la “Usiku wa Msanii” lafanyika
tarehe 25-Oct-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Marehemu Father Kanuti
alipewa tuzo ya Humanitarian Award.
•Tarehe 09-Dec-2014, siku ya maadhimisho ya miaka 53 ya
Uhuru na miaka 52 ya Jamhuri ya Tanganyika (Tanzania Bara), Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla maalum iliyofanyika katika
viwanja vya ikulu atoa nishani maalum kwa kundi zima la Atomic Jazz Band ya
Tanga. Tuzo hiyo ni ya miaka 50 ya Muungano ya daraja la nne. Aliyepokea kwa
niaba ya kundi ni mzee Stephen Hiza (Mgosingwa). Atomic Jazz Band imepewa
nishani hiyo kutokana na kazi yao kubwa katika kulihamasisha taifa kuenzi
muungano hususan kwa kupitia wimbo wao wa
“Tanzania Yetu”.
•Mpambano wa Msondo na Sikinde wafanyika mara mbili kwa
kuandaliwa na Fred Ogot na kampuni yake ya Bob Entertainment. Mara ya kwanza
ulifanyika siku ya sikukuu ya Eid Mosi (Eid al-Fitr) tarehe 25-Jul-2014 ndani
ya TCC Chang’ombe. Mara ya pili umefanyika pia TCC Chang’ombe Christmas tarehe
25-Dec-2014. Kwenye mpambano wa mara ya pili, kwa mara ya kwanza tukio
limesindikizwa na bendi ya Vijana Jazz Pambamoto “Saga Rumba”.
•MAONYESHO YA PAMOJA: Bendi 3 za FM Academia, Mapacha
Watatu na Ruby Band zapiga pamoja Ijumaa ya tarehe 19-Dec-2014 ndani ya
Mzalendo Pub. Yamoto Band mara kadhaa imefanya maonyesho ya pamoja kwa kupiga pamoja
na Mapacha Watatu, Skylight Band na Twanga Pepeta. Pia Mlimani Park Orchestra
wamepiga pamoja mara kadhaa na Machozi Band ya Lady Jaydee. Ruby Band walipiga
pamoja na Twanga Pepeta Jumapili ya tarehe 28-Dec-2014 ndani ya Leaders Club
•Onyesho la Miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga
Pepeta lililokuwa lifanyike Jumamosi ya tarehe 20-Dec-2014 limeahirishwa hadi
tarehe 31-Jan-2015 kutokana na kifo cha mnenguaji Aisha Madinda.
•Mechi ya mpira wa miguu kati ya kundi la BONGO DANSI na
kundi la WATANASHATI WA MUJINI lafanyika katika viwanja vya Leaders Club
Jumapili ya tarehe 23-Nov-2014. Matokeo yalikuwa suluhu 0-0. Kundi la BONGO
DANSI mara kadhaa limefanya ziara ya kumtembelea Nguza Vicking na Papii Kocha
ambao wapo gerezani Ukonga.
•Tarehe 26-Dec-2014, umoja wa wanamuziki wa dansi
katika viwanja vya Karimjee wafanya dua maalum ya kumuombea Rais Jakaya Kikwete
ili hali yake ya kiafya iimarike.
No comments:
Post a Comment