Afisa Masoko wa Airtel
Henrick Bruno akionyesha moja kati ya vocha za Airtel UNI255 maalum kwa vyuo
vikuu nchini tayari kwa uzinduzi jumamosi hii.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
· Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole
kupamba uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UDSM
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii
itazindua rasmi huduma mpya maalum kwaajili ya kutoa huduma nafuu za
mawasiliano kwa wanafunzi walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es salaam
UDSM ambapo hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Airtel UNI
255 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika viwanja vya
Mabibo hostel
Akiongea
kuhusiana na uzinduzi wa huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando
amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa
wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa
wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye
mtandao huduma hiii ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake
kwenye inteneti, kupiga simu na hata sms. Huduma hii tayari tumeshaizindua kwa
vyuo vikuu vingine vya Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza na imeonyesha mafanikio
makubwa sana kwa watumiaji wakiwemo wanafunzi na wale wote wanaotumia huduma
hii maeneo ya vyuo”
“Airtel
tumeona ni vyema tuizindua hapa katika vyuo vya Dar es salaam wiki hii siku ya
Jumamosi pale mabibo hostel ambapo mbali na uzinduzi kutakuwa na tamasha kubwa
litakalopambwa na watoa burudani nguli akiwemo Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki,
Shilole pmaoja na DJ maarufu jiji Dj Zero aliongeza kusema Mmbando
Nae
meneja wa huduma hiyo ya UNI 255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana hii ni
huduma maalum kwa wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema kuizindulia katika
Hostel zao pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi wengi wa chuo kikuu hapa
jijini wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo wanakaribishwa katika uzinduzi huo
ambapo kiingilo chake ni BURE”
Burudani
zitakuwa zakutosha kupitia Airtel UNI 255 siku hiyo.
Kampuni ya simu za mkononi ya airtel ilianzisha huduma ya
UNI255 ili kuendana sambamba na mkakati wao wa kusaidia vyuo vikuu nchini
kutumia ipasavyo huduma za mtandao ili kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la
kusaidia wateja wake walioko vyuoni kufikia malengo yao.
No comments:
Post a Comment