AMAVUBI watakaokuja nchini Januari 21 kucheza na Stars Maboresho |
Stars maboresho wanaotarajiwa kuvaana na Amavubi Januari 22 |
Tayari Kocha Mkuu wa Stars, Mart Nooij ameteua kikosi cha wachezaji 26 wa timu hiyo kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Januari 22, mwaka huu.
Nooij alisema kati ya wachezaji hao 10 ambao
wanatoka katika mikoa ya kanda ya ziwa wataweka kambi Mwanza na wengine 10
wanaotoka upande wa Dar es Salaam wataweka kambi hapo Dar es Salaam.
Alisema
kambi
kwa ajili ya michuano hiyo itaanza rasmi kesho Jumapili na siku
inayofuata watakwenda Mwanza kuungana na wengine kwa ajili ya kambi ya
pamoja.
“Mechi hiyo
ni muhimu kwetu kwani wachezaji ambao watafanya vizuri tutawapandisha kucheza
katika kikosi kikubwa,”alisema Nooij.
Nooij aliwataja wachezaji wa kikosi hicho kuwa ni; Aishi
Manula, Benedict Tinoko, Miraji Adam, Andrew Vicent, Michael Gadiel, Emmanuel
Semwanda, Joram Mgeveke, Edward Charles na Adam Salamba.
Wengine ni; Aboubakary Mohammed, Hassan Dilunga,
Hussein Malombe, Shiza Ramadhani, Omari Nyenje, Kelvin Friday, Alfred
Masumbakenda, Salim Mbonde, Atupele Green na Rashid Mandawa.
Pia wamo Manyika Peter,
Salum Telela, Hassan Banda, Mohammed Hussein, Said Ndemla, Said Makapu na Simon
Msuva.
Aidha,
kwa mujibu wa taarifa ya Mjumbe wa Kamati
Tendaji ya Shirikisho la Soka Tanzani (TFF), Vedastus Lufano, kiingilio kwenye
mechi hiyo itakuwa sh. 20,000 kwa viti maalumu (VIP), viti vya kawaida sh.
10,000 na mzunguko ni sh. 3,000.
Lufano
aliwataja baadhi ya wachezaji wa Amavubi wanaotarajia kutua jijini Mwanza
Januari 21 kwa ndege ya Rwanda Air, kuwa ni Marcel Nzarora, Olivier Kwizera,
Sotel Kayomba, Ismail Nshutiyamagala , Emery Basiyenge na Michel Rushengoga.
Wengine ni Fitina Ombolenga, Janvier Mutijima, Haruna Niyonzima, Tean Baptista,
Mugiraneza Savio, Nshuti Dominique, Patrick Sibomano, Jean Claude, Zagabe
Andrew, Buteara Ernest , Sugira Danny, Ushengimana Betramed Iladukunda na
Blenvue Mugenzi.
Lufano aliongeza kuwa taarifa iliyotumwa TFF kutoka Rwanda, Amavubi itaongozana
na viongozi waliotajwa kuwa ni Stephen Costan, Vincent Mashami, Ibrahim
Mugisha, Moussa Hakizimana, Nuhu Assouman, Boume Mugabe, Piere Baziki na Mkuu
wa Msafara Bandora Felician.
Awali,
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) Boniface Wambura
alisema mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo
kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN).
Mechi za
mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda
zinaanza Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment